Na Gift Mongi;Moshi.

Maandalizi yote ya mkutano wa baraza la umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi(UVCCM)Moshi Vijijini tayari yamekamilika na kinachosubiriwa hivi sasa ni siku yenyewe.

Miongoni mwa maandalizi yenyewe ni pamoja na eneo la ukumbi lakini pia kuwataarifu wajumbe ambao wapo maeneo mbali mbali ya wilaya hiyo.

Akitoa taarifa hiyo kwa  wanahabari mwenyekiti wa umoja wa vijana wa chama cha mapinduzi (UVCCM)wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenail Shirima anasema hatua zote muhimu zimeshafikiwa na kuwa wajumbe wajitokeze kwa wingi.

'Ninachotaka kusema hapa ni kuwa mambo ya msingi yameshakamilika na wajumbe wajitokeze kwa wingi katika baraza letu hili muhimu kwa ustawi wetu lakini na chama kwa ujumla wake'amesema

Kwa mujibu wa Shirima ni kuwa mkutano huo utafanyika julai mosi katika ukumbi  CCM wilaya ya Moshi Vijijini na kuwa wajumbe halali wa baraza  hilo hawapaswi kukosa 

'Kama mwenyekiti nitumie fursa hii adimu kuwakaribisha wajumbe hawa katika mkutano huo na utakumbuka sisi ndio jeuri ya chama na alipo mama vijana tupo'anasema

Estomihi Urio ambaye amewahi kuwa kiongozi wa UVCCM miaka ya tisini amesema baraza hilo lina nguvu katika chama na kuwa limekutwa likitumika.kuwaandaa viongozi

'Ukiwa mjumbe wa baraza  la UVCCM hiyo ni njia mojawapo katika kuwaandaa viongozi wakubwa serikalini lakini pia ndani ya chama'amesema

Share To:

Post A Comment: