Na John Walter-Kiteto


Mkuu wa Wilaya ya Kiteto,Mhe. Mbarak Batenga, amewataka wakazi wa Wilaya hiyo kuchangamkia fursa mbalimbali zinazotokana na ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi kutoka Hoima Uganda hadi Chongoleani Tanga ( EACOP), ambalo litapita wilayani hapo.

Akifungua semina ya EWURA kwa wafanyabiashara, mafundi, watoa huduma na wananchi wa Kiteto kuhusu kuzitambua fursa na namna ya kujisajili kwenye kanzidata ya EWURA, leo Juni 6,2023, Mhe. Batenga amewasishi wadau hao kuhamasika kujisajili ili waweze kutoa huduma na utaalamu kwenye mradi huo wa EACOP.

EWURA huwasajili bila malipo kwenye kanzidata https://cqs.ewura.go.tz/
watanzania wenye sifa ya kutoa huduma mbalimbali kwenye miradi ya mafuta na gesi asilia nchini.


 
Share To:

Post A Comment: