NA FARIDA MANGUBE.

Zaidi ya wakazi 6,900 wa kata ya Mbingu Halmashauri ya MLIMBA mkoani Morogoro wanatarajiwa kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na Salama utakapo kamilika mradi mkubwa wa Maji Mbingu ambao kwa awamu ya Kwanza unagharimu Takribani shilingi Milioni 760.

 Mradi huo unaotekelezwa na Serikali chini ya Wakala wa Maji Safi na usafi wa Mazingira vijijini (RUWASA) ni Kati ya Miradi sita iliyopitiwa na Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 kwenye halmashauri ya MLIMBA na kuwekewa jiwe la msingi na kiongozi wa Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Ndg.Abdalla Shaib Kaim.

Akisoma Taarifa ya Mradi wa Maji Mbingu Kaim Meneja RUWASA wilaya ya Kilombero Mhandisi Florence Mlelwa amesema mradi huo umefikia asilimia 95 katika utekelezaji wake na utakapo kamilika utamaliza kabisa shida ya maji katika eneo Hilo na kuwawezesha wakazi wake kuendelea na shughuli za uzalishaji.

Akiwa katika Mradi wa maji Mbingu kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Abdulla Shaib Kaim amesema ameridhishwa na utekelezaji wa Mardi na matumizi ya fedha.

"Niwapongeza Sana ndugu zangu RUWASA kwa kazi kubwa na zuri unayoifanya ya kuhakikisha wananchi waishio vijiji wanapata maji Safi na salama.alisema Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Morogoro ,Fatma Mwassa amesema Bil. 12.1 zimetumika katika kutekelezaji wa miradi 68 itakayotembelewa Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri 9 za Mkoa huo. 
Share To:

Post A Comment: