Serikali ya Mkoa wa Shinyanga imewataka waajili wa sekta binafsi kufuata kanuni na taratibu zilizopo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wafanyakazi wanalipwa stahiki zao kwa wakati.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga baada ya kupokea changamoto kutoka shirikisho la wafanyakazi TUCTA Mkoa wa Shinyanga kwenye maadhimisho ya sherehe za wafanyakazi Mei Mosi ambayo kimkoa yamefanyika katika Wilaya ya Kishapu.

Katika risala iliyosomwa na mratibu wa TUCTA Mkoa wa Shinyanga Bwana Ramadhan Pangara ametaja baadhi ya changamo zinazowakabili wafanyakazi Mkoani Shinyanga huku akiiomba serikali kushughulikia.

“Changamoto zinazotukabili sisi wafanyakazi wa Mkoa wa Shinyanga katika Utumishi wa Umma na pia wafanyakazi wa Sekta Binafsi kama ifuatavyo baadhi ya waajiri wa Sekta Binafsi kutozingatia sheria, Kanuni, taratibu na miongozo inayotolewa na serikali”

”Jambo hili imesababisa changamoto zifuatazo kutotolewa kwa Mikataba ya ajira na Waajiri, kuwazuia wafanyakazi kutojiunga vyama au kuachisha kazi Wale wanaojiunga na vyama vya wafanyakazi jambo ambalo ni kinyume na sheria ya Ajira na Mahusiano kazini sura ra 366 rekebisho la 2019, baadhi ya Waajiri hawawachangie watumishi wao au hawapeleki michango kwa wakati kwenye mifunko ya hifadhi ya jamii, baadhi waajiri hawatoi hati za malipo ya Mishahara kwa Wafanyakazi, waajiri binafsi kutozingatia waraka wa Mishahara wa mwaka 2022, kwa kima cha chini, ambao utekelezaji wake umeanza Januari 2023”.amesema mratibu Pangara

“Tunaiomba Serikali isimamie kwa ukaribu sana taratibu za ajira katika sekta binafsi kama ilivyo katika sekta ya Umma ucheleweshwaji wa Mafao ya Kustaafu kwa wafanyakazi kutoka Katika Mifuko ya Hifadhi ya Jamil imeendelea kuwa changamoto kubwa kwa wastaafu wengi ambao warnelitumikia Taifa hili kwa uadilifu kwa muda mrefu. Baadhi Ya wastaafu warnejikuta wakipoteza maisha hata kabla hawajalipwa mafao yao ya kustaafu. Tunaomba wastaafu wetu walipwe mafao yao mara tu baada ya kumaliza likizo yao ya mwisho ya kustaafu”

“Madai mbalimbali ya Uhamisho, Mapunjo ya Mishahara Malipo Ya nauli za likizo, Matibabu na gharama za masomo imekuwa kero kubwa hasa kwa watumishi katika sekta ya Umma japo malipo haya yanafanyika lakini si kwa wakati na kwa kiwango ambacho kingewamotisha wafanyakazi hawa Tunaomba sana serikali ya awamu ya Sita ichukue hatua madhubutj kuondoa kabjsa kero hizi ikiwa ni pamoja na kulipa nauli kabla mtumishi hajaenda likizo ya malipo.”.amesema mratibu TUCTA

“Waajiri wa Sekta za Umma na binafsi kutozingatia na kudhoofisha haki za kioganaizesheni za wafanyakazi Jambo hili limesababisha mambo yafuatayo, kutozingatiwa kwa Mikataba ya Utambuzi na Majadiliano ya pamoja, Kutofuatwa kwa masharti yanayounda mabaraza ya Wafanyakazi na hata kwa baadhi ya waajiri sekta za Umma hasa Halmashauri kutofanya Mabaraza ya Tathmini baadhi ya waajiri kutotoa wafanyakazi hodari ama kutenga bajeti ndogo kwa ajili ya kuwamotisha wafanyakazi”

“Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Trade Union Congress of Tanzania) TUCTA kwa niaba ya wafanyakazi wote wa Mkoa wa Shinyanga tunapenda kutumia fursa hii kukushukuru kwa moyo wa dhati, kupokea na kukubali mwaliko wetu na kushiriki nasi katika siku hii ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) ambayo Kimkoa inafanyika hapa Wilaya ya Kishapu tunasema asante sana”

“Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Mkoa wa Shinyanga linawakilishwa na jumla ya Vyama shiriki vipatavyo kumi ambavyo ni COTWU (T), CWT, CHODAWU, TAMICO, TALGWU, TEWUTA, TUGHE, TUICO, TPAWU na RAAWU”

“Tunaungana na Watanzania wote kuipongeza kwa dhati serikali ya awamu ya Sita kwa juhudi nyingi zinazofanywa katika Taifa letu kama kuboresha mahusiano ya kitaifa na kimataifa, kuweka mazingira mwafaka kwa wawekezaji, kuitangaza Nchi kimataifa, kuongeza Ajira katika utumishi wa Umma, na kuendelea kusimamia vyema utekelezaji wa Miradi ya Kimkakati katika Nchi yetu”

“Katika Maadhimisho ya Mei Mosi mwaka huu 2023 yenye Kauli Mbiu Isemayo "Mishahara Bora na Ajira za Staha ni Nguzo kwa maendeleo ya Wafanyakazi" Wakati ni Sasa! Kauli mbiu hii imetokana na hali halisi ya maisha ya wafanyakazi kutokana na uwepo wa Mishahara midogo na Maslahi duni yasiyokidhi hali na gharama za maisha kwa sasa”

 “Hivyo tunaiomba Serikali na wamiliki wa Makampuni binafsi pamoja na Viwanda wazingatie Uboreshaji wa Mishahara na Maslahj kwa wafanyakazi wa Nchi ili iendane na gharama halisi za Maisha”.amesema mratibu Pangara

“Aidha, tunaendelea kusisitiza waajiri wote watoe Mikataba ya ajira inayokidhi viwango Wa kisheria, kufanya Majadiliano ya pamoja (Mikataba ya Hali Bora, Mabaraza ya Wafanyakazi) ili kutatua changamoto zilizopo na kupunguza migogoro sehemu za kazi na hatimaye kupatikane Tija na Ufanisi katika sehemu za kazi”

 Kwa upande wake Mwenyekiti wa TUCTA Mkoa wa Shinyanga Bwana Mathias Balele  ameipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo ameiomba serikali kufanya kikao cha pamoja ili kutatua changamoto zilizopo ikiwemo ile ya Kikokotoo.

“Ni kweli watumishi wetu wamekuwa wakipata shida sana kwa sababu sheria haieleweki kwa wanachama wetu kwa mfano tuliambiwa kwenye kikokotoo kulingana na kanuni mafao ya mwisho wa mwezi yataongezeka lakini tunayo mifano kuna wafanyakazi wetu waliostaafu Miaka miwili kwa daraja lilelile kwahiyo tunaiomba serikali ikae meza moja na shirikisho la vyama vya wafanyakazi wakae meza moja na mawaziri wakaangalie upya kanuni hizi zipate kuwabeba watumishi wetu wa Tanzania”.amesema Mwenyekiti Balele

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewataka waajili katika sekta binafsi kuzingatia sheria huku akimwagiza katibu tawala wa Mkoa wa Shinyanga kufuatilia ili kubaini taasisi za umma zinazokiuka sheria za kazi na maelekeozo ya serikali.

“Madai ya watumishi wa umma na sekta binafsi yakiwemo ya likizo, uhamisho na malimbikizo ya mshahara niwatake waajili wa sekta binafsi kuhakikisha wanawalipa madai watumishi kwa wakati na kwa upande wa serikali watumishi wa umma maelekezo yamekwisha tolewa watumishi wa umma wasihamishwe bila kulipwa stahiki zao”

“Niwatake waajili kuhakikisha kuwa mnatenga fedha kwenye bajeti zetu kwa ajili ya likizo na stahiki zote za watumishi kuhusu baraza la wafanya kazi katika sekta za umma kutofanya vikao vya mabaraza ya wafanyakazi na kutolipa stahiki zao kwa mujibu wa sheria ninakuagiza katibu tawala wa Mkoa wa Shinyanga ufuatilie hili na uniletee orodha ya taasisi za umma zinazokiuka walaka wa serikali’”.amesema RC Mndeme

RC Mndeme ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kuendelea kushirikiana na serikali katika kutokomeza ukatili unaoendelea huku akisisitiza jamii hasa wazazi na walezi kusimamia maadili mema kwa watoto ili kuwaepusha na mmomonyoko wa maadili ikiwemo kujiingiza kwenye makundi mabaya na wengine kwenda kinyume na mila na desturi za Nchi.

Pia mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewaomba wananchi kuendelea kushirikiana na vyombo vya usalama kwa kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu unaofanywa na baadhi ya watu wenye nia mbaya katika Mkoa huo.

Amewaangiza viongozi wenye mamlaka katika serikali za mitaa Mkoa wa Shinyanga kuweka utaratibu wa kaya kutopokea wageni pasipo kutolewa taarifa kutoka kwenye uongozi wa vitongoji na vijiji ili kuimarisha usalama na kwamba hali hiyo itasaidia kuendelea amani ya Nchi.

Akitoa salam kwa niamba ya wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Shinyanga, mkuu wa Wilaya ya Kishapu Bwana Joseph Mkude ametumia nafasi hiyo kuwasihi wafanyakazi kutimiza wajibu wao kila mmoja katika nafasi yake bila kujali changamoto zinazowakabili huku akiwasisitiza kuepuka migogoro hasa sehemu za kazi ambapo amewahimiza kufanyakazi kwa upendo, umoja, kuheshimiana pamoja na kushirikiana ili kuendeleza tunu ya Taifa.

Sherehe za maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani Mei mosi katika Mkoa wa Shinyanga imefanyika katika uwanja Mwadui Complex Wilaya ya Kishapu na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa na serikali na taasisi binafsi  ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa  Shinyanga Bi. Christina Mndeme.

Katika Maadhimisho ya Mei Mosi Mwaka huu 2023 kitaifa yamefanyika Mkoani Morogoro kauli Mbiu inasema "MISHAHARA BORA NA AJIRA ZA STAHA NI NGUZO KWA MAENDELEO YA WAFANYAKAZI" Wakati ni Sasa!

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza kwenye maadhimisho ya sherehe za siku ya wafanyakazi mei mosi katika uwanja wa Mwadui Complex uliopo Wilaya ya Kishapu.

Mwenyekiti wa TUCTA Mkoa wa Shinyanga Bwana Mathias Balele akizungumza kwenye maadhimisho ya sherehe za siku ya wafanyakazi  mei mosi  katika uwanja wa Mwadui Complex uliopo Wilaya ya Kishapu.

Mratibu wa TUCTA Mkoa wa Shinyanga Bwana Ramadhan Pangara  akisoma risala kwenye maadhimisho ya sherehe za siku ya wafanyakazi mei mosi  yaliyofanyika kimkoa katika Wilaya ya Kishapu.

Akitoa salam kwa niamba ya wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Shinyanga, mkuu wa Wilaya ya Kishapu Bwana Joseph Mkude leo katika maadhimisho ya mei mosi.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga upande wa kulia Mhe. Johari Mussa Samizi, mkuu wa Wilaya ya Kahama katikati Mhe. Mboni Mhita pamoja na Mstahiki meya wa Manispaa ya Shinyanga upande wa kushoto Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko wakiwa katika maadhimisho ya Mei mosi  yaliyofanyika katika uwanja wa Mwadui Complex Wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga.

Mratibu wa TUCTA Mkoa wa Shinyanga Bwana Ramadhan Pangara akitambulisha wageni waliohudhuria maadhimisho hayo.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko upande wa kushoto wakiwa katika maadhimisho Mei mosi katika uwanja wa Mwadui Complex Wilayani Kishapu.

Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ya Mei mosi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme

 

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme na Mwenyekiti wa TUCTA Mkoa wa Shinyanga Bwana Mathias Balele upande wa kulia wakiwa katika maadhimisho ya sherehe za siku ya wafanyakazi mkoani humo.

Katibu tawala wa Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo akitambulisha viongozi wa serikali waliohudhuria sherehe hiyo ya Mei mosi Mkoani Shinyanga.

Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe. Mboni Mhita .

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Mussa Samizi.

Viongozi mbalimbali wa serikali akiwepo Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Dkt. Jomaary Satura wakiwa katika sherehe za siku ya wafanyakazi Mkoani Shinyanga.

Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa katika zoezi la kukabidhi vyeti na zawadi kwa wafanyakazi bora kutoka kwenye Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga.

Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa katika zoezi la kukabidhi vyeti na zawadi kwa wafanyakazi bora kutoka kwenye Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga.

Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa katika zoezi la kukabidhi vyeti na zawadi kwa wafanyakazi bora kutoka kwenye Halmashauri za Mkoa wa Shinyanga.

Tazama picha za mabango yenye ujumbe mbalimbali juu ya maadhimisho ya sherehe za siku ya wafanyakazi Duniani ambapo Mkoawa Shinyanga  imefanyika katika Wilaya ya Kishapu.


Share To:

Misalaba

Post A Comment: