TAZAMA VIDEO HII.

 Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

Shilingi Bilioni 6.7 (6,705,107, 554. 34) zimetolewa na serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kutekeleza zaidi ya miradi 19 ya maendeleo katika jimbo la Shinyanga mjini kwa Mwaka wa fedha 2023.

Akizungumza na Baraza la umoja wa wanawake wa Tanzania UWT Wilaya ya Shinyanga mjini lililojumuisha viongozi wa CCM na jumuiya nyingine za chama hicho Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu  Paschal Patrobas Katambi amesema fedha hizo ni kwa ajili ya kuhitimisha mwaka wa fedha 202\2023.

Fedha hizo zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muugano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani ambapo Mbunge Mhe. Katambi amesema zimeelekezwa kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo hasa katika ujenzi wa miundombinu katika sekta za elimu na afya.

Mbunge huyo amefafanua kuwa  fedha hizo zitatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga ikiwemo ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule kongwe, elimu bila ada kwa shule za msingi na sekondari, ukamilishaji wa vyumba vya madarasa kwa shule za msingi, ujenzi wa bweni katika shule za sekondari, ujenzi wa vyoo katika shule shikizi, ujenzi wa bweni shule maalum za msingi.

Amesema zitatumika pia katika ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za sekondari, ujenzi wa nyumba za walimu shule za msingi, fedha za mitihani, ujenzi wa Hospitali za wilaya, ukamilishaji wa zahanati, vifaa tiba kwenye vituo vya afya, fedha za UNICEF, fefha za mfuko wa afya wa pamoja HSBF, ujenzi wa majengo ya Halmashauri, ujenzi wa nyumba za wakurugenzi pamoja na mfuko wa kuchochea maendeleo ya jimbo CDCF.

Jumla ya Shilingi Bilioni 6.7 zimeletwa katika jimbo la Shinyanga Mjini kwa  ajili ya utekekelezaji wa miradi ya maendeleo na shughuli zingine katika sekta za elimu, afya, utawala na mfuko wa kuchochea maendeleo ya jimbo kwa kipindi cha robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2022/2023.

Jumla ya shilingi Bilioni 3.3 (3,357,091,104.34)  zimeelekezwa katika sekta ya elimu ambapo fedha hizo zitajenga vyumba vipya vya madarasa, matundu ya vyoo, mabweni, mabwalo ya chakula na nyumba za walimu.

 Aidha, katika sekta hiyo ya elimu fedha hizo zitagharamia utolewaji wa Elimu Msingi bila Malipo pamoja na shughuli za uendeshaji mitihani ya Taifa katika Shule za Msingi na Sekondari.

Katika sekta ya Afya, jumla ya Bbilioni  1.4 ( 1,454,424,450) zitatumika katika ujenzi wa Hospitai ya Wilaya, ukamilishaji wa zahanati, ununuzi wa vifaa tiba katika vituo vya afya, fedha za kugharamia mfuko wa afya ya wa pamoja (HSBF) na fedha za shirika la afya duniani UNICEF.

Idara ya Utawala, Fedha na Rasilimawatu jumla ya Bilioni 1.8 (1,831,898,000) zimetengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Majengo ya Ofisi za Halmashauri, ujenzi wa nyumba za wakurugenzi na matumizi mengineyo.

Jumla ya kiasi cha shilingi milioni 61,694,000 zimeelekezwa katika mfuko wa kuchochea maendeleo ya jimbo (CDCF) la Shinyanga Mjini.

Adha katika semina hiyo iliyojumuisha viongozi mbalimbali washiriki wamefundishwa kuhusu dhana ya uongozi na maadili.

Maada zilizofundishwa ni pamoja na  majukumu muhimu ya uongozi, itifaki na utaratibu, nafasi ya UWT kuelekea uchaguzi, mikakati ya UWT ya kuimalisha Chama, nafasi ya uongozi na watendaji na mwelekeo wa UWT, mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto na sheria haki na wajibu.

Mwenyekiti huyo Bi. Rehema Nhamanilo amesema mafunzo ya semina hiyo yatasaidia kuendelea kuimarisha jumuiya ya umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi UWT Wilaya ya Shinyanga mjini huku akimshukuru na kumpongeza (Mgeni rasmi), Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu  Paschal Patrobas Katambi kwa kuendelea kuleta matokeo chanya ya maendeleo katika jimbo hilo.

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu  Paschal Patrobas Katambi akizungumza kwenye semina hiyo.

Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini naibu waziri ofisi ya waziri Mkuu kazi,vijana,ajira na wenye ulemavu  Paschal Patrobas Katambi akizungumza kwenye semina hiyo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa  wanawake wa chama cha mapinduzi CCM, UWT Wilaya ya Shinyanga mjini Bi. Rehema Nhamanilo akizungumza kwenye semina hiyo.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa  wanawake wa chama cha mapinduzi CCM, UWT Wilaya ya Shinyanga mjini Bi. Rehema Nhamanilo akizungumza kwenye semina hiyo.

Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Shinyanga Grace Samwel akizungumza kwenye semina hiyo ambayo imefanyika katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mhe. Anord Makombe akizungumza kwenye semina hiyo ambayo imefanyika katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Shinyanga mjini.


Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Mussa Samizi akitoa maada kwenye semina hiyo iliyoandaliwa na umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi CCM, UWT Wilaya ya Shinyanga mjini.

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Mussa Samizi akizungumza kwenye semina hiyo iliyoandaliwa na umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi CCM, UWT Wilaya ya Shinyanga mjini.

Mjumbe wa Baraza la UWT Taifa Bi. Christina Gule akitoa maada kwenye semina hiyo

Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Bwana Ally Shabani Ally awali akitambulisha viongozi wa chama kwenye semina hiyo.


Katibu wa itikadi, siasa na uenezi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Said Bwanga akitoa maada kwenye semina hiyo iliyolenga kuendeneza umoja wa UWT Wilaya ya Shinyanga mjini.

Katibu wa itikadi, siasa na uenezi CCM Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Said Bwanga akizungumza kwenye semina hiyo iliyolenga kuendeneza umoja wa UWT Wilaya ya Shinyanga mjini.


Mwezeshaji kutoka dawati la jinsia na watoto Wilaya ya Shinyanga Bi. Jane Mwanzembe akitoa maada ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika semina iliyoandaliwa na  UWT Wilaya ya Shinyanga mjini

Mwezeshaji kutoka dawati la jinsia na watoto Wilaya ya Shinyanga Bi. Jane Mwanzembe akitoa maada ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto katika semina iliyoandaliwa na  UWT Wilaya ya Shinyanga mjini

Katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga Bi. Asha Kitandala akitoa maada kwenye semina iliyoandaliwa na UWT Wilaya ya Shinyanga mjini.

Katibu msaidizi wa mkoa wa Shinyanga Bi. Halima Makologanya akitoa maada kwenye semina iliyoandaliwa na UWT Wilaya ya Shinyanga mjini.

Mjumbe wa Baraza la UWT Mkoa wa Shinyanga Bi. Hamisa Magulu akitoa maada kwenye semina iliyoandaliwa na UWT Wilaya ya Shinyanga mjini.

Katibu wa UWT Wilaya ya Shinyanga Mjini Bi. Lucy Enock akizungumza kwenye semina hiyo. 




Mbunge wa jimbo la Msalala Mhe. Iddi Kassim Iddi mbele akiwa kwenye semia hiyo.


Share To:

Misalaba

Post A Comment: