Na, Bertha Mollel, Arusha. 

Benki ya NMB imefanikiwa kutoa msaada wa madawati 100 kwa shule ya msingi Msasani iliyoko Muriet nje kidogo ya jiji la Arusha ambapo inatarajiwa kukaliwa na wanafunzi zaidi ya 50.

NMB imetoa msaada huo iliyoenda sambamba na uzinduzi wa tawi jipya la 'kwa Mrombo' iliyoko katika kata ya Muriet kwa lengo la kusongeza karibu huduma za kifedha ambazo zimekuwa changamoto kubwa kwa wananchi wa eneo hilo la pembezoni mwa mji.

Akizungumza katika uzinduzi wa tawi hilo la kwa Mrombo, na makabidhiano ya madawati hayo kwa mkuu wa mkoa, kaimu mkurugenzi wa NMB Filbert Mponzi alisema madawati hayo ni sehemu ya kurudisha shukrani kwa jamii inayowapa sapoti kubwa katika mafanikio waliyonayo.

"Tawi hili tunalofungua leo ni la 229 huku tukiwa na amana ya zaidi ya trillion 3.3 ambazo ni fedha za mafanikio yaliyochagizwa na jamii ndio maana huwa tunatoa misaada hii kurudisha shukrani kwao lakini zaidi kuwapa huduma rafiki"

Pia alisema kuwa kwa mwaka huu wa 2023 benki yao wameanzisha kampeni ya utunzaji wa mazingira ambayo wamedhamiria  kupanda miti milioni moja nchi nzima lengo ikiwa ni kuunga jitihada za serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabia ya nchi iliyoathiri wananchi wengi msimu uliopita.

Mmoja wa wanafunzi waliopokea madawati hayo kwa niaba ya wenzake wa shule ya msingi Msasani, Juma Mussa alisema kuwa msaada huo utawasaidia kupunguza adha ya kukaa wengi kiti kimoja huku akiwaomba wadau wengine kujitokeza kuwasaidia.

Akizindua tawi hilo, mku wa mkoa wa Arusha John Mongela alisema kuwa sehemu kubwa ya uchumi wa Tanzania unategemea ukuaji wa Sekta ya kifedha hasa utoaji wa huduma bora na rafiki kwa wananchi wake na taasisi mbali mbali za uwekezaji.

"Mmefanya kazi nzuri na kubwa inayohitaji pongeza kwa kusogeza huduma ya kifedha eneo hili maana naamini mbali na wananchi kunufaika na huduma za kifedha lakini pia mtatoa elim ya matumizi ya utunzaji rasilimali hii eneo salama ambayo ni benki" alisema Mongela na kuongeza..

"Niendelee kutoa shukrani zangu za dhati kwenu kwani mmekuwa msaada mkubwa wa kuisadia Serikali hasa katika sekta ya elim na afya kwa misaada yenu ya vifaa mbali mbali na Mimi ni shuhuda katika maeneo mengi tuliyokabidhiana hivyo nitoe wito kwa benki zingine kuiga mfano huu"

Mmoja wa wakazi wa eneo la 'kwa Mrombo' Julius Laizer alisema kuwa kusogezwa kwa huduma hiyo utasaidia kupunguza uhalifu wa uporaji ambao umekuwa ukifanyika sana hasa siku za mnada wanapouza mifugo na mazao lakini pia vikundi vya Vikoba na Saccos ambao baada ya kukusanya fedha hulazimika kusafiri hadi mjini kwa ajili ya kuhifadhi.

Share To:

Post A Comment: