Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Mkoani Singida Miraji Jumanne Mtaturu amekabidhi mifuko 400 ya saruji katika Shule ya Sekondari Dr Shein kama ishara ya kuanza rasmi kwa ujenzi wa mabweni ya wanafunzi kwani imekuwa kikwazo cha elimu bora kwa wanafunzi wanaotoka mbali kwenda kupata elimu shuleni hapo.

Sambamba na hilo mbunge huyo pia amekabidhi vifaa mbalimbali vya mafunzo  Computer 4 na projector 1 kwa ajili ya mafunzo ya TEHAMA kwa wanafunzi kuunga mkono kampeni ya serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia ya Tanzania ya kidigitaliShare To:

Post A Comment: