MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ameishukuru serikali kwa kuendelea kutekeleza miradi ya maji kwenye vijiji vinne vilivyopo Wilayani Ikungi Mkoani Singida ikiwa ni jitihada za kuhakikisha huduma ya maji inafika kwa wananchi.


Vijiji hivyo ni Minyinga, Mkunguwakihedo,Sakaa na Matare.


Pamoja na shukrani hizo,ametaka kujua ni lini serikali itahakikisha umeme unawekwa katika mradi wa maji kwenye kijiji cha Matare kilichopo jimbo la Singida Mashariki ili wananchi wapate maji.


Akiuliza swali Mei 2,2023,bungeni Jijini Dodoma,Mtaturu amesema serikali imefanya kazi nzuri ya kupeleka miradi ya maji kwenye vijiji hivyo vinne.


“Katika vijiji hivi nilivyovitaja serikali imeweka miundimbinu ya maji,ila kijiji cha Matare kilichopo Jimbo la Singida Mashariki mkandarasi amemaliza kujenga mradi huo ila kikwazo ni umeme,na TANESCO wameshalipwa gharama za kuunganisha umeme lakini bado hawajaunganisha,Je ni lini serikali itahakikisha umeme unaunganishwa ili wananchi wa Matare waweze kupata maji,?”amehoji Mtaturu.


Akijibu swali hilo,Waziri wa Maji Jumaa Aweso amemuhakikishia mbunge Mtaturu kuwa suala hilo watalifuatilia kwa ukaribu ili kuhakikisha ujenzi unakamilika na wananchi wanapata maji.


“Wizara ya Maji inafanya kazi kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na wamekuwa msaada mkubwa kwetu,nikuhakikishie Mbunge Mtaturu kwamba jambo hili tutalifuatilia kwa ukaribu ili kuhakikisha ujenzi wa eneo hilo unakamilika kwa haraka,”amesema.

Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: