WAF - Arusha

Wizara ya afya kwa kushirikiana na Shirika la afya Duniani (WHO) wameendesha Mafunzo ya kwanza  kwa watoa huduma za afya nchini kwa lengo la kuweka mipango midogo  ili kufanikisha uwekezaji wa miongozo ya kupambana na magonjwa ambayo hayapewi kipaumbele kuanzia ngazi ya jamaii.

Akizungumza leo jijini Arusha kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Serikali  Mkurugenzi wa mafunzo na rasiliamali watu Wizara ya Afya, Dkt. Saitole Laizer amesema  mafunzo hayo yanalenga jamii kushiriki kwenye kuweka mikakati mahususi ya kutokomeza magonjwa yasiyopewe kipaumbele.

Katika mpango mkakati unaonzia 2021 mpaka 2026 Tanzania imefanikiwa  kupambana na magonjwa yasiyopewa kipaumbele ambapo kwa ugonjwa wa vikope kwa halmashauri 77 zilikuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi na kwa sasa 9 ndio zinahitaji afua ya kumezesha dawa kinga ili kutokomeza maambukizi ya ugonjwa wa vikope.

Pia Dkt. Saitole ameeleza kuwa ugonjwa wa matende na mabusha Halmashauri 119 zilikuwa na kiwango kikubwa cha maambukizi lakini mpaka sasa halmashauri 9 ndio zinahitaji afua ya kumezesha dawa kinga ili kutokomeza maambukizi ya ugonjwa huo.

Naye Meneja Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Magonjwa yasiyopewa kipaumbele kutoka Wizara ya Afya, Dkt. George Kabona amebainisha magonjwa yasiyopewa kipaumbele kuwa ni Vikope, kichocho,Minyoo ya Tumbo, Usubi, Matende na Mabusha.

Aidha amesema kuwa halmashauri 9 ndio zinahitaji afua ya kumezesha dawa kinga za kutokomeza maambukizi ya ugonjwa vikope ni Ngorongoro, Monduli, Longido,Kitete, Simanjiro, Mpwapwa, Chamwino, Kongwa na Karambo.

Vile vile amesema halmashauri za Kinondoni, Temeke, Ilala, Pangani, Mafia, Kilwa na Mikindani ndo zinahitaji afua ya kumezesha dawa kinga za kutokomeza ugonjwa wa Matende na mabusha

Dkt. Kabona ameeleza kuwa mafunzo hayo yameshirikisha  nchi tisa zikiwemo Kenya,Uganda, Ethiopia, Malawi, Mozambique, Eretria.

Share To:

Post A Comment: