Na Okuly Julius-Dodoma

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt.Jim Yonazi ametoa Wito kwa Wakurugenzi wote nchini, Makatibu Tawala kuhakikisha kwamba wanasimamia vizuri Mradi Wa Programu ya kuendeleza kilimo na Uvuvi Katika maeneo yao."Lakini pia Maafisa Viungo ninyi ndio watendaji wakuu na ni watekelezaji kabisa, kuhakikisha kwamba mambo haya tunayoyatazamia yanatekelezwa kwa uhakika" amesema Yonazi.Ameyasema hayo leo Mei 04,2023 Jijini Dodoma alipokuwa akifungua Warsha ya Utambulisho na Uelewa wa Programu hiyo kwa Watendaji wa Mikoa na Halmashauri.


Yonazi amewataka watekelezaji kwenye Taasisi husika kuhakikisha Mradi huo unafanikiwa kwa wakati pasipo kukwama njiani."Ninyi ni watekelezaji wa kitaalamu, mmepewa Fedha hizi pamoja na vifaa Ili kazi hizi ziweze kutekelezwa vizuri" amesema Yonazi.


Katibu Mkuu huyo amesema Programu hiyo itawezesha ujenzi, ukarabati na ukaguzi wa miundombinu ya vituo vya kuendeleza vizazi vya viumbe Maji kama kile Kinguluwila-
Morogoro,Lubambagwe- Geita na itakarabati miundombinu ya Mabwawa.

Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu wa shughuli za Serikali Bw. Paul Sangawe.


Naye Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Uratibu wa shughuli za Serikali Bw. Paul Sangawe amesema katika Programu hiyo wanatazamia Meli zitanunuliwa kwa upande wa Tanzania bara na Visiwani zitakazo wezesha nchi kwa mara ya kwanza kuweza kufanya uvuvi katika Bahari Kuu Ili kuweza kutumia rasilimali ambazo kwa ufanisi.


Sangawe amesema Lengo kubwa la mkutano huo ni kuutambulisha Programu hiyo kwa watendaji hao wa Mikoa na Halmashauri Ili kuweza kujua majukumu yao na pia Vile vile waweze Kufuatilia utekelezaji wa Programu na kuhakikisha kwamba Fedha ambazo wamepewa Mkopo Wa Dola Milioni 58.8 zinatumika kwa Ufanisi na malengo yaliyokusudiwa.
Share To:

OKULY BLOG

Post A Comment: