NA FARIDA MANGUBE, 


Watu wanne wa familia moja Kijiji cha Malola B Kata ya Malola Tarafa ya Mikumi Wilaya ya Kilosa Mkoani Morogoro wamefariki baada ya nyumba waliokuwa wakiishi kuungua Moto usiku wa kuamkia Mai 5, 2023.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, ACP Alex Mkama amefika eneo la tukio na kuthibisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema bado uchunguzi unaendele ili kubaini chanzo cha tukio Hilo.

Aidha Kamanda amewataja waliofariki ni Amani Malekela (72) ambaye ni Baba wa familia hiyo, Habiba Aman ( 10), Sadick Amna (8) na Bahati Aman( 5)


Share To:

Post A Comment: