NA OR-TAMISEMI


WAKUU wa mikoa yote Tanzania Bara wamepewa elimu juu ya biashara ya hewa ukaa nchini ambayo itasaidia kuongeza mapato na kuimarisha utoaji wa huduma kwenye mamlaka za Serikali za Mitaa.

Hayo yameelezwa leo Aprili 3, 2023 jijini Dodoma katika kikao cha pamoja kilichoongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI),Mhe. Angellah Kairuki na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dkt. Selemani Jafo.

Akizungumza katika kikao hicho, Mkurugenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Andrew  Komba amesema biashara ya kaboni ni uwezo wa msitu wa Kitropiki au Asili kunyonya tani za hewa ukaa ambapo tunapata maksi katika utunzaji wa mazingira yaani (Carbon Credit).

Amesema, utunzaji wa misitu mikubwa unawezesha kunyonya hewa ya kaboni kwenye anga, hivyo kupunguza athari kwenye tabaka la ozone ambalo linaathirika kutokana na msongamano wa hewa ya ukaa linalosababishwa na uwepo wa viwanda vikubwa duniani, matumizi ya magari yanayotumia Petroli na Diseli, pamoja na matumizi ya kuni na uchafuzi mwingine wa mazingira.

Amesema, biashara ya Kaboni ina masoko makubwa ya aina mbili yaani soko la hiari pamoja na Soko la Umoja wa Mataifa ambalo ni lazima kwa wenye viwanda vikubwa duniani kuhakikisha wanatunza mazingira kwa kulipia misitu yenye uwezo wa  kupunguza hewa ukaa.

Naye Afisa Mazingira kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bi.Hawa Mwechaga amesema, kati ya Halmashauri zinazonufaika na biashara ya hewa ukaa ni Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika ambapo wanepata shilingi Bilioni 7.8 kwa kipindi cha miaka 3 na kwa mwezi Novemba wamepata shilingi Bil.4.2 ambazo zinawasiaida katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Kwa sasa kanuni na muongozo wa uendeshaji wa biashara ya hewa ukaa zimeshaandaliwa ambazo zitasimamian biashara hii kwenye Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka  za Serikali za Mitaa.

Share To:

Post A Comment: