Wa katikati ni katibu tawala wilaya ya Nachingwea Omari Said Mwanga akikabidhi mpira wa zawadi mbele ya OCD wa wilaya ya Nachingwea James Chacha wakati wa kufunga Mashindano ya Polisi jamii Cup
Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Nachingwea James Chacha akiongea wakati wa kufunga Mashindano ya Polisi jamii Cup




Na Fredy Mgunda, Nachingwea.

MAJENGO FC mabingwa wapya wa Polisi jamii Cup wilaya ya Nachingwea baada ya kuifunga timu ya Veteran FC kwa goli moja kwa bila(1-0) katika fainali iliyofanyika kwenye uwanja wa shule ya msingi Majengo. 

Mashindano ya Polisi jamii Cup yameandaliwa na Jeshi la Polisi wilaya ya Nachingwea chini ya usimamizi wa Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Nachingwea James Chacha kwa lengo la kuimarisha umoja na mshikamano baina ya Jeshi la polisi na jamii ili kurahisisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao. 

Akizungumza wakati wa kufunga Mashindano hayo Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Nachingwea James Chacha alisema kuwa wamefanya Mashindano hayo kwa lengo la kutoa elimu kwa jamii hasa vijana juu ya umuhimu wa kutunza amani na kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi wilaya ya Nachingwea.

Chacha alisema kuwa Mashindano hayo yalihusisha mashindano ya mpira wa miguu ambayo yamehusisha timu nne ambazo ni Bodaboda Fc, Majengo Fc, Ajax Fc, Veteran Fc na Lion Fc ambapo timu ya Majengo Fc imeibuka kuwa bingwa na kujinyakulia zawadi za seti ya jezi, mbuzi na mpira huku nafasi ya pili ikishikiliwa na klabu ya Veteran Fc na kupata zawadi ya seti ya jezi na mpira mmoja na nafasi ya tatu imechukuliwa na Lion Fc waliojipatia zawadi ya mpira mmoja

Kwa upande wake mgeni rasmi wa fainali ya Polisi jamii Cup,Katibu tawala wilaya ya Nachingwea Omari Said Mwanga ameitaka jamii kushirikiana vizuri na Jeshi la polisi ili kuhakikisha amani iliyopo kwa muda mrefu inalindwa. 

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: