Na Elizabeth Paulo Dodoma


Filamu ya Tanzania ya The Royal Tour Imeongoza filamu zingine zote kwa asilimia 80% Ambapo watu bilioni 1.2 wamejihusisha na filamu ikiwemo kuijua, kuiskia, kuiona au kuifuatilia TANZANIA kutokana na ROYAL TOUR.


 Leo jijini Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati ya Rais ya Kuitangaza Tanzania Kimataifa, Dkt. Hassan Abbasia amesema amesema Watanzania wanatakiwa kuchangamkia fursa zitokanazo na faida iliyopatikana kutokana na Filamu ya Royal Tour ambapo watalii milioni 3.8 wametembelea vivutio vya utalii mwaka uliopita. 


Amesema watalii milioni 1.45 wanatoka nchi mbalimbali duniani huku watalii milioni 2.36 wakiwa ni watalii wa ndani wanaotembelea vivutio mbalimbali vya utalii.




“Tunaendelea kuimarisha utalii Kaskazini mwa Tanzania na tunafungua utalii Kusini mwa Tanzania, nawaomba Watanzani wenzangu tuchangamkie fursa zitokanazo na Royal Tour, unaweza kuwekeza hata katika vikundi vya utamaduni kama vile vikundi vya ngoma asilia na usukaji wa vikapu, watalii wanapenda sana vitu vya asili,” ameeleza Dkt. Abbasi.


Amesema watalii waliotembelea maeneo mbalimbali nchini wameongeza mapato yatokanayo na sekta hiyo kutoka Shilingi trilioni 3.301 mwaka 2021 hadi Shilingi trilioni 5.8 mwaka 2023.


Pamoja na hilo, Dkt. Abbasi amesema wawekezaji kutoka mataifa ya nje wamevutiwa kuwekeza nchini ambapo mikataba nane yenye thamani ya Shilingi trilioni 11.7 imesainiwa huku miradi ya utalii ikiongezeka kutoka 16 kabla ya kurushwa Filamu ya Royal Tour hadi 26 mwaka huu.


Kwa mujibu wa Ripoti ya Waandaaji wa ROYAL TOUR, filamu hii si tu imeshaoneshwa katika vituo zaidi ya 300 vya Runinga vilivyoko kwenye majimbo (States) zote za Marekani, lakini tofauti na ROYAL TOUR nyingine zote, filamu ya Tanzania imetajwa kuwa namba 1 kwa kutazamwa zaidi na vituo vingi vya runinga kulazimika kuirudia na vinaendelea Kuirudia.


Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: