Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Deogratius J. Ndejembi amesema Serikali imeshaanza matengenezo katika barabara ya Kibaoni, Endala, Endamariek hadi Endabash ambapo Katika mwaka wa fedha wa 2021/22, Serikali ilipeleka Shilingi Milioni 599.97 kwa ajili ya ujenzi wa daraja lenye urefu wa mita 40 kwenye barabara hiyo na ujenzi wake umekamilika.

Amesema hayo leo tarehe 17 Aprili 2023  Bugeni Dodoma wakati akijibu Swali la Mbunge wa Jimbo la Karatu, Mhe. Daniel Awack Tlemai aliyetaka kujua je, ni lini barabara ya Kibaoni, Endala, Endamariek hadi Endabash itajengwa.

Amesema katika mwaka wa fedha wa 2022/23, Serikali imetenga Shilingi Milioni 68 kwa ajili ya matengenezo ya sehemu korofi yenye urefu wa kilomita 5 katika barabara hiyo na utekelezaji wake unaendelea.

Aidha, Ndejembi amesema katika Mwaka wa Fedha wa 2023/24, Serikali itatenga Shilingi Milioni 213.02 kwa ajili ya kujenga madaraja mawili (2), matengenezo ya sehemu korofi yenye urefu wa kilomita 10 pamoja na matengenezo ya muda maalum yenye urefu wa kilomita 2 katika barabara hiyo.

Share To:

Post A Comment: