Na John Walter-Manyara

Mkuu wa mkoa wa Manyara Mhe. Charles Makongoro Nyerere amewataka wananchi mkoani humo na maeneo ya Jirani kuhudhuria katika uzinduzi wa maadhimisho ya wiki ya chanjo duniani yatakayofanyika katika uwanja wa Kwaraa Mjini Babati  siku ya Jumatatu  April 24,2023 kuanzia asubuhi.

Taarifa ya mkuu wa mkoa imesema tukio hilo litaambatana na shuguli mbalimbali zikiwemo upimaji wa Afya na utoaji chanjo za magonjwa mbalimbali bure.

Kauli mbiu ni "Tuwafikie wote kwa chanjo"

Mkuu wa mkkoa amesema katika maadhimisho hayo, Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu.

Amewataka wananchi wote wahudhurie kwenye tukio hilo muhimu akisema  "jamii iliyopata chanjo ni jamii yenye afya"

Wiki ya chanjo imetengwa maalum kwa ajili ya kuhimiza umuhimu wa chanjo kwa Watoto wenye umri chini ya miaka 5 na wasichana wenye umri kuanzia miaka 14 ili kuwakinga na maradhi mbalimbali hasa homa ya ini, surua na polio na wasichana wenye umri kuanzia miaka 14 kwa ajili ya chanjo ya kinga ya saratani ya shingo ya kizazi.

 

Share To:

Post A Comment: