Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chamwino, Mhe. Deogratius J. Ndejembi ametoa wito kwa Viongozi wa dini na Watanzania Wote kuendelea kumuombea Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kazi Kubwa anayoendea kufanya ya kuleta maendeleo na kudumisha amani, Umoja na mshikamano kwa Watanzania.


Ndejembi ameeleza hayo Aprili 19, 2023 katika futari Maalum aliyoiandaa kwa ajili ya Viongozi wa dini pamoja na Viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya Chamwino kwa ajili ya dua ya kumuombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika futari hiyo, Ndejembi ametumia fursa hiyo kueleza kazi kubwa inayoendelea kuifanywa na Rais Dkt. Samia kwa Wananchi wa Wilaya Chamwino na Watanzia wote ambapo ameeleza miradi mingi iliyotekelezwa sekta ya elimu, afya, maji, umeme na miundombinu mbalimbali.

Nao, Viongozi wa dini ya Kiislam na Kikristo waliongoza dua na maombi Maalum kwa Taifa la Tanzania huku wakimuombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan afya njema na maarifa ya kuelendelea kuliongoza Taifa la Tanzania.
Share To:

Post A Comment: