Mgombea nafasi ya ujumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM anaewakilisha Mkoa wa Arusha NAMELOK SOKOINE ameishinda nafasi hiyo kwa kura 39 kati ya kura 67 zilizopigwa na kuwabwaga wagombea wenzake 8.

Hussein Gonga alikuwa mshindi wa pili kwa kupata kura 16 akifuatiwa na Dr. Daniel Palangyo aliyekuwa akitetea nafasi yake hiyo ambapo alipata kura 5. 

Msimamizi wa uchaguzi huo Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda  baada ya kumtangaza MNEC huyo aliwaasa wajumbe wa Mkoa Arusha kuendelea kukijenga chama baada ya uchaguzi huku akikemea tabia ya baadhi ya wagombea kutumia majina ya viongozi wa juu serikalini na kwenye chama kuomba nafasi za uongozi.

MNEC wa mkoa wa Arusha Namelock Sokoine ameahidi   kushirikiana na chama kuhakikisha chama kinaendelea kushika dola..

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Zelothe Stephen amewashukuru washiriki wote kugombea nafasi ya UNEC na sasa uchaguzi umekwisha cha msingi nikurudi kukijenga chama.

Share To:

Post A Comment: