Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na mkuu wa wilaya ya Liwale Goodluck Mlinga kwa ajili ya kuanza kukimbizwa wilayani humo
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akiwa na viongozi mbalimbali pamoja na vijana wa hamasa wakati wa kuupokea Mwenge wa Uhuru mwaka 2023

Na Fredy Mgunda, Nachingwea.



MKUU wa Wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo amesema kuwa Mwenge wa Uhuru mwaka wa 2023 utakagua miradi ya kimaendeleo yenye thamani ya shilingi billion 1.4  katika wilaya hiyo ikiwa fedha kutoka serikali kuu, mapato ya ndani na michango ya Wananchi.

Akiupokea Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 kutoka wilaya ya Liwale, Moyo alisema kuwa Mwenge wa Uhuru utambelea Mradi wa uwezeshaji wa vijana kiuchumi  wenye thamani ya Tsh Milioni 15, ujenzi wa Barabara kiwango Cha Lami Y2K Kwa Milanzi, Kwa Milanzi hadi Voda na Polisi Kuelekea mianzini wenye thamani ya Tsh Mil 480 , ujenzi wa OPD, Maabara , Jengo la kufulia na kichomea taka vyenye thamani ya Tsh Milioni 900 , ujenzi wa madarasa manne Shule ya Msingi Majengo yenye jumla ya Tsh Milioni 80 


Alisema kuwa miradi mingine ambayo itatembelewa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu ni kama vile chanzo Cha maji na uhifadhi wa Mazingira Ruponda , Shughuli za mapambano dhidi ya Rushwa na mapambano dhidi ya madawa ya kulevya.

Hivyo mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa wameupokea Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 utakinginzwa kwa amani na utulivu mkubwa,shangwe nyingi kutoka kwa wananchi mbalimbali za wananchi wa wilaya hiyo.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: