Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi akiongea na waandishi wa habari kuhusu matukio mbalimbali yaliyojitokeza mkoa humo.
Madawa ya kulevya aina ya Heroin aliyokamatwa nayo mtu mmoja anaijukikana kwa jina la Rashid
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Iringa ACP Allan Bukumbi akionyesha sila ambayo ilitelekezwa Misitu ya SAO HILL


Na Fredy Mgunda, Iringa.


JESHI la Polisi mkoa wa Iringa linamshikilia Mwasema Rashid mkazi wa Tabata Magengeni jijini Dar es Salam kwa kosa la kugundulika kuwa kete 58 za madawa ya kulevya aina ya Heroin tumboni mwake.

Katika taarifa ya kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Allan Bukumbi kijana huyo amekamatwa baada ya kuumwa tumbo na hivyo kwenda zahanati ambapo alibainika kuwa na madawa hayo .

"Tarehe 31 machi 2023 mtuhumiwa huyo akiwa safarini kurudi Jijini Dar es Salam majira ya saa Tano usiku wilaya ya kilolo Mkoa wa Iringa katika Kijiji Cha Mtandika alianza kujisikia vibaya na kuamua kufika zahanati ya Mtandika na kujieleza na daktari huku hali ikiendelea kuwa mbaya ndipo alipoamua kusema ukweli " Alisema Bukumbi 

Alisema kuwa Mwasema Rashid aligundulika kuwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin  aliyokuwa akisafirisha kuelekea nchini Msumbiji baada ya kuitumia usafiri wa anga .

Kamanda ACP Bukumbi alisema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na hali mbaya tarehe 2 mwezi wa nne ambapo hali ilibainika na kuwa mbaya na kumsaidia kutoa kete 58 kwa njia ya haja kubwa chini ya uangalizi wa madaktari na Jeshi la polisi .

Kupitia taarifa hiyo kijana Macdonald Zuberonga (23) mkazi wa Semtema  na Hatuna mbigili (24 ) mkazi wa wa ipogolo walikutwa na madawa ya kulevya yadhaniwayo kuwa ni bhangi kete (324) na majani makavu aina ya bhangi ambayo yalikutwa sehemu wanazoishi .

katika hatua nyingine silaha aina ya shortgun yenye namba za usajili TZCAR 88980  ilikutwa imetelekezwa katika vichaka vya msitu wa saohil wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa .

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: