KATIKA Kutekeleza agizo la Rais Samia Suluhu Hassan kusogeza huduma za kibingwa kwa wananchi Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI), imepeleka huduma za kibingwa  ijulikanayo kama Mobile Kliniki kwa wakazi wa Mbagala.

Katika Kliniki hiyo iliyofanyika leo katika Hospitali ya Epiphany iliyopo Mbagala Kuu, zaidi wananchi 500 walijitokeza kupata huduma.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Taasisi ya Epiphay, Pharles Yikobela aliishukuru  MOI kwa kuwa mstari wa mbele kuunga mkono juhudi za Rais Samia.

“Leo tuko na madaktari kutoka MOI wamekuja kwa ajili ya kliniki tuna madakatari bingwa wa mifupa, mgongo na mishipa ya fahamu na ubongo, napenda kumshukuru Raisa wetu mama Samia Suluhu Hassan ambaye amewekeza kwa kiasi kikubwa upande wa afya,” amesema.

Amesema wamejenga hospitali ambayo inatoa huduma mbalimbali na nzuri na wamewekeza vizuri, hivyo wananchi watumie fursa hizo  kwani vipimo vinafanyika na matibabu yanatolewa.

Yikobela amesema matatizo ya mifupa yako kwa asilimia kubwa, ambapo pia yapo katika magonjwa yanaoongoza hivyo kikubwa ni kuelimisha na kufuata sheria za usalama barabarani.

“Tunaomba hospitali zingine za juu kuja huku chini kutujengea uzoefu kwa madaktari katika hospitali mbalimbali, ili kumuunga mkono Rais Samia kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kibingwa,” amesema.

Amebainisha kuwa kupitia kliniki hiyo wana mambo mengi ya kujifunza  na itawajenga uwezo madaktari wao wa ndani kwa kupata ujuzi kutoka MOI.

“Tutaiga mfano huu tutaenda chini kutoa huduma kama hii tunapenda hili zoezi kuwa endelevu angalau kila baada ya miezi miwili  ili kuwahudumia wananchi wa Mbagala ambao wengi wao vipato vyao viko chini,”amesisitiza Yikobela na kuongeza kuwa:

“Na tunaona kwamba gharama za kumuona daktari bingwa ni Sh 10,000  lakini ukienda MOI gharama inazidi hiyo  na kama wagonjwa wote wakienda MOI patajaa, lakini huduma zikipatikana hapa inakuwa rahisi jamii inapata huduma katika mazingira ambayo wananchi wanakaa.”

Mratibu wa Kliniki Jongefu (mobile clinic) kutoka MOI,  Dk Byrason Mcharo amesema mwaka jana walianzisha kliniki na wametembelea hospitali mbalimbali, huku   lengo ni kuwa na gari ambayo itakuwa na huduma zote za mifupa, ubongo na mishipa ya fahamu

Amesema zoezi hilo limeanzia mkoa wa Dar es Salaam na wanategemea kwenda Pwani na Morogoro lakini pia wana kliniki ambayo inatwa ‘outreach’ ambayo sahivi iko mikoa ya Tabora, Mtwara, Lindi ambapo wanataka huduma zienda kila mkoa Tanzania.

“Mwitikio wa watu ni mkubwa kwa mara ya kwanza tulienda Hospitali ya Zakhiem na tuliona watu zaidi ya 400 na Watanzania wanakubali huduma,”ameeleza

Share To:

Post A Comment: