Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania (DPP) amemfutia kesi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya JATU PLC, Peter Gasaya, aliyekuwa anakabiliwa na mashtaka ya kujipatia Sh5.1 bilioni kwa njia ya udanganyifu.

Hiyo ni baada ya kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, leo Jumanne April 11, 2023.

Gasaya amefutiwa kesi hiyo chini ya kifungu namba 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai (CPA), sura ya 20, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Share To:

Post A Comment: