Na; Elizabeth Paulo, Dodoma 


Wananchi waaswa kuwekeza katika bunifu pamoja na kuwasapoti wabunifu wakitanzania kwa kununua bidhaa zao na kuwapa mrejesho mzuri ili kuwatia moyo ikiwa ni katika kuthamini jitihada zao.


Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu tume ya taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH) Dr.Amosi Nungu wakati akizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni wiki ya Ubunifu kitaifa ambapo wabunifu mbalimbali wanapata nafasi ya kuonyesha bunifu zao katika kiwanja cha jamuhuri jijini Dodoma.


Aidha amesema kuwa kwa mwaka huu wamekuwa tofauti kidogo kwani wameboresha kwani kuna siku maalumu kwaajili ya taasisi zote lakini kikubwa ni kwamba COSTECH tumeweza kuwasidia wabunifu wa nyuma kuweza kuingia sokoni na kuweza kunufaika na bunifu zao."Niwaombe watanzania tuwatie moyo wabunifu wetu wanaopambana kila kukicha kubuni vitu ambavyo vitasaidia kuondoa changamoto katika jamii na mkivitumia kama kuna upungufu au kasoro utabaini usiache kuwarejeshea maoni ya kurekebisha ili ubunifu huo uweze kutumika kwa manufaa ya watanzania na taifa kwa ujumla,"Amesema Dr. Nungu


Na Kuongeza"Kama COSTECH tumesaidia wabunifu mbalimbali mfano mzuri kijana mbunifu wa mita ya maji sasahivi amepewa tenda na RUWASA kufunga mita nchi nzima kwa hivyo niwaambie tu vijana wanaweza kupata ajira kupitia bunifu zao,Haitoshi kwa mfano katika MAKISATU yaliyopita kuna kijana alibuni gari ya kutumia mfumo wa umeme lakini alivyokuja kwetu tukabaini mapungufu na tukamdhamini kwa kumpatia kiasi cha shilingi milioni 10 ili akaboreshe yale mapungufu'.amesema Dkt.Nungu


Aidha ameongeza kuwa Serikali inajukumu la kuweka mazingira wezeshi kwa wabunifu lakini haya maonyesho yanaangali zaidi Ubunifu kwa upana wake na ndomaana tunawasihi wananchi, taasisi mbalimbali, wanafunzi wa shule za msingi,sekondari na vyuo kuja kujifunza kubwa zaidi kuwekeza katika hizi bunifu.
"Wananchi wengi wanadhani kwamba bunifu za Tanzania hazidumu yaani tunazionea haya kuzitumia lakini kuona ndo kuamini mfano bunifu ya gari ya kutumia umeme sisi kama taasisi ni kutoa ushauri na maelekezo ili kuweza kuboresha zaidi na kuaminiwa na wananchi"


Aidha ameongeza kuwa vijana wanapaswa kuwa na uthubutu wa kubuni bunifu zenye manufaa kwa jamii na ili kuwapa fursa wananchi kujifunza kutoka kwenye bunifu hizo ili kuhamasisha vijana wengine wanaochipukia kwenye bunifu kuja na mbinu nyingine nzuri zaidi na kufanya wananchi kuzidi kuwa na imani na wabunifu wazawa kwa kuwapa sapoti ya kutosha na ushirikiano wa kudumu.


"Tumeona bunifu nyingi tu hapa zinazofanywa na vijana zikiwa na utofauti mkubwa sana na bunifu zingine hii ni kuonyesha ni kwa kiasi gani kama nchi tunakuwa katika sekta hii haswa ukizingatia namna ambavyo vijana wanaweza kujiajiri lakini kutoa elimu kisasa na kwenda na wakati haswa kwa wanafunzi mashuleni"Amesisitiza Dr.Amos


Aidha ametoa wito kwa vijana kuacha kukopi bunifu za wengine na kubuni kitu cha utofauti ili kuweka rekodi ya kipekee kama kijana kwa kuwa wa kwanza kubuni bunifu ya kipekee na yenye tija na kuleta ushawishi kwenye jamii.


Sambamba na hilo Dk.Nungu amesema kuwa kuna kila sababu ya vijana wa kitanzania kutambua na kuamini juu ya ubunifu unaofanywa nchini Tanzania badala ya kusifia bunifu za nje ya nchi."Kwa sasa serikali kupitia COSTECH imeweza kuwaweka sokoni vijana wengi ambao wameonekana kuwa wabunifu kwa kuwapatia vibali vya kuwaendeleza na kuwajengea uwezo wa kiuchuni jambo ambalo linaendelea kutoa hamasa katika jamii",Na kuongeza kuwa "Vijana wengi ambao wanajitokeza kwa kujitambulisha kuhusu ubunifu walionao wamekuwa wakisaidiwa kwa kuendelezwa au kuunganishwa katika mashirika mbalimbali ambayo yanakuwa yana uwezo wa kiutendaji kulingana na ubunifu alio uonyesha,"amesema Dkt.NunguKuhusu wabunifu ambao wanabuni vifaa ambavyo ni hatarishi kama vile gobore au bunduki amesema kuwa wanatakiwa kuwasiliana na COSTECH kabla ya kuingia sokoni kwa kuuza bidhaa hizo.Amesema kuwa serikali kazi yake kubwa ni kuwawezesha na kuwajengea uwezo wabunifu ambao wanaonekana kubuni vifaa hatarishi kwa kulinda usalama wa nchi na siyo kazi ya serikali kuwakamata na kuwaweka ndani.Maonesho hayo yameandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa lengo la kuwakutanisha wabunifu mbalimbali ambapo wanatumia kama jukwaa la kuonesha bidhaa zao mpya ambazo wamezibuni kupitia Taasisi zao ili jamii ione na kuvichukuwa kwa ajili ya kwenda kuvitumia kwa kutatua changamoto zao na kurahisisha utendaji katika shughuli za kila siku.Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: