Ferdinand Shayo ,Kilimanjaro. 


Zaidi ya Wakulima 300 wa ngano kutoka mikoa ya Kilimanjaro,Manyara na Arusha wamepatiwa mafunzo juu ya matumizi sahihi ya mbolea ya kuchanganya na mbegu  aina ya YaraVita Seedlift inayotumika kustawisha mazao hasa katika kipindi cha ukame na kumuwezesha mkulima kuwa uhakika wa mavuno kwa asilimia 75% licha ya mabadiliko ya tabia ya nchi. 

Akizungumza na Wakulima hao katika Shamba darasa la Ngano Wilayani Siha.Afisa Kilimo kampuni ya Yara  kanda ya kaskazini  Novatus Salala amesema kuwa mbolea hiyo ni mkombozi kwa wakulima hasa katika kipindi hiki ambacho maeneo mengi nchini yanakabiliwa na uchache wa mvua. 

Afisa kilimo Halmashauri ya Siha Habibu Ally ameipongeza kampuni ya Yara kwa kutoa elimu kwa wakulima juu ya matumizi sahihi ya mbolea zinazozalishwa na kampuni hiyo kwa lengo la kuwasaidia wakulima kupata uhakika wa mavuno. 

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha Dancan Urassa  ameyataka mapuni mengine kuiga mfano wa kampuni ya Yara katika kutoa elimu ya kilimo bora cha ngano kwa wakulima wa mikoa ya Arusha,Kilimanjaro na Manyara. 

Kwa upande wao wakulima wa ngano Bertha Akiyoo na Melijoh Laizer wamepipongeza kampuni ya Yara kwa kuwakutanisha pamoja na kuwapatia elimu ya matumizi ya mbolea ambayo tayari imeanza kuleta matokeo makubwa kwa wakulima wakubwa na wadogo. 

"Mbolea hii imekuja wakati muafaka ambao kuna uhaba wa mvua kwani ina uwezo wa kustawisha ngano na kumpatia mkulima uhakika wa mazao" Alisema  Bertha Akiyoo.

Share To:

Post A Comment: