Mwenyekiti
wa TUGHE tawi la Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Nuwia Sultan (kulia aliyeshika
boksi) akikabdhi msaada wa vitu mbalimbali kwa Msaidizi wa Gereza la Wanawake
Isanga, Mrakibu Msaidizi wa Magereza Yuster Ligazio wakati wanawake watumishi
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi walipowatembelea Gereza Kuu Isanga Dodoma na kukabidhi msaada huo kwaajili ya wafungwa, mahabusi wanawake na watoto wao
katika Gereza hilo. Msaada huo ni sehemu
ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani inayoadhimishwa Duniani kote Machi 8
ya kila mwaka.
Wanawake
watumishi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakiwa na Maafisa Magereza baada ya
kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwaajili ya wafungwa, mahabusi wanawake na watoto wao katika
Gereza Kuu Isanga jijini Dodoma. Msaada
huo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani inayoadhimishwa Duniani
kote Machi 8 ya kila mwaka.
Post A Comment: