Afisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Lilian Mwelupungwi akielezea umuhimu wa kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia wakati wa uzinduzi wa siku ya mwanamke duniani
Kushoto ni Monica chaula afisa NMB katikati ni Hadija nalinga afisa mahusiano NMB na mwisho kulia ni afisa ustawi wa jamii wilaya ya Nachingwea Lilian Mwelupungwi wakipanda mti isha wa uzinduzi wa siku ya wanawake duniani katika wilaya hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo akipanda mti ishala ya utunzaji wa mazingira katika uzinduzi wa siku ya wanawake duniani iliyofanyika hii leo katika shule ya sekondari ya Nachingwea girls

Na Fredy Mgunda, Iringa.

WANAWAKE wa Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea Mkoani Lindi wanapinga vitendo vya ukatili wa kijinsia vinavyofanywa na baadhi ya wanaume ambavyo vimekuwa vikiwazalilisha wanawake na watoto wa wilaya ya Nachingwea.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa siku ya wanawake wilaya ya Nachingwea, afisa maendeleo ya jamii Lilian Mwelupungwi alisema kuwa wamekuwa wakitoa elimu ya ukatili wa kijinsia mara kwa mara kupitia vyombo vya habari na makundi maalum.


Mwelupungwi alisema kuwa Polisi na taasisi mbalimbali zimeunda madawati ya kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa jamii yote ya wilaya ya Nachingwea na kutoa elimu na kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria ambavyo vimekuwa vikichukua maamuzi kulingana na sheria za nchi zinavyotaka.

 Alisema kuwa kila mwananchi wa wilaya ya Nachingwea wamekuwa mstari wa mbele kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ili jamii iendee kuwa na maadili kwa faida ya maendeleo ya Taifa.


Mwelupungwi alisema kuwa wanaendeleza kutoa elimu kwa wanaume juu ya madhara ya vitendo vya ukatili kwa Watoto na wanawake.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa  aliwataka wanawake wa wilaya ya Nachingwea kuacha Mara moja tabia ya kuogopa na kupaza sauti juu ya vitendo ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake,wazee na watoto ambao umekua unatokea dhidi yao.

Moyo ameyasema hayo alipokua kwenye uzinduzi wa wiki ya wanawake ambao wamezindua kwa kupanda miti kwenye shule ya sekondari ya wasichana Nachingwea


Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: