Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Severa Salvatory akizungumza na wakuu wa shule na maafisa Elimu wa Halmashauri za Mkoa huo kwenye kikao cha kufanya tathmini ya maendeleo ya Elimu kilichofanyika Mjini Kibaha
Baadhi ya walimu wakuu wa shule,maafisa elimu msingi na Sekondari Mkoani Pwani wakiwa kwenye kikao cha tathinini ya maendeleo ya Elimu kilichofanyika Kibaha Mkoani Pwani , wadau hao wameiomba Serikali  kuajiri walimu wa Elimu maalumu msingi na wengineo ili kundi hilo nalo lifikiwe .   Picha Juliet Ngarabali.
Baadhi ya walimu wakuu wa shule,maafisa elimu msingi na Sekondari Mkoani Pwani wakiwa kwenye kikao cha tathinini ya maendeleo ya Elimu kilichofanyika Kibaha Mkoani Pwani , wadau hao wameiomba Serikali  kuajiri walimu wa Elimu maalumu msingi na wengineo ili kundi hilo nalo lifikiwe .   Picha Juliet Ngarabali.


Julieth Ngarabali ,Kibaha


Wadau wa elimu wameiomba Serikali   kuongeza ajira za walimu wa Elimu maalumu nchini  ili kuwezesha  watoto wenye ulemavu wa aina mbalimbali kupata fursa ya kijifunza kuanzia elimu ya awali,msingi na kuendelea kwa ukamilifu kama ilivyo kwa  wengine wasio na changamoto hiyo.


Ombi hilo limetolewa  na wadau hao huko  Mjini Kibaha Mkoani Pwani waliohudhuria  kikao cha wakuu wa shule, maafisa Elimu  Msingi na sekondari  kutoka Halmashauri zote  Mkoani humo chenye  lengo la kufanya tathmini ya maendeleo ya Elimu kwa miezi mitatu kuanzia  Januari hadi Machi mwaka huu.


"Hili kundi nalo ni muhimu kupata elimu lakini changamoto uhaba wa walim mfano tu s isi Halmashauri ya Bagamoyo tuna upungufu wa walimu 12 wa elimu maalumu maana waliopo ni 17 tu, "amesema Wema Kajigili.


Kajigili ambaye ni Afisa Elimu awali na Msingi Wilayani Bagamoyo amesema changamoto hiyo ni vema ikafanyiwa kazi kwa wakati kwani walimu hao wanaumuhimu hasa kukuza uelewa kwa wanafunzi wenye ulemavu ikiwemo uziwi katika kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK)


Naye  Afisa Elimu taaluma Halmashauri ya Chalinze Hamisi Shemahonge amesema  uuwiano wa walimu wa Elimu maalumu hauendani na mahitaji jambo ambalo linawapa ugumu wanafunzi wenye uelemavu wakati wa kijifunza.


Awali akifungua kikao hicho , Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani Severa Salvatory aliwataka wadau hao  kutekeleza majukumu yao kikamilifu  na kujiwekea malengo ikiwemo kupambana na changamoto zilizopo kwani lengo ni kuhakikisha kundi hilo nalo linapata elimu.


"Fanyeni vikao mara kwa mara kulingana na miongozo iliyopo Ili kupata tathmini na mwenendo wa kazi na kama kuna changamoto mnazifanyia kazi kwa wakati"amesema.


Aidha Afisa Elimu Mkoa wa Pwani Sara Mlaki  amewaelekeza Maafisa hao  pamoja na wakuu wa Shule  kuhakikisha wanaifanyia kazi changamoto ya kuondoa tatizo la baadhi ya wanafunzi wasiojua kusoma na kuandika maarufu (KKK)  Ili kukuza kiwango cha elimu.


Mlaki amesema  taarifa alizopata ni kwamba hali hiyo inachangia na wanafunzi wanaohamia kutoka mikoa mingine wanakuwa na tatizo hilo hivyo ni vema wakabainishwa Ili kupata   ufumbuzi wa kukabiliana nalo.


Sekta ya elimu na mafunzo kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 na Mpango wa muda mrefu wa maendeleo ya Taifa 


Sekta ya elimu na mafunzo, kwa mujibu wa Dira ya Maendeleo 

ya Taifa ya 2025 na Mpango wa muda mrefu wa Maendeleo 

ya Taifa  2011/12 hadi 2024/25, inatarajiwa kuleta maendeleo 

ya haraka ya rasilimaliwatu kwa kutayarisha idadi ya kutosha 

ya Watanzania walioelimika na kupenda kujielimisha zaidi ili 

kulifanya Taifa lipate maendeleo na kuwa lenye uchumi wa kati na shindani ifikapo mwaka 2025. 


Mwisho

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: