Na,Jusline Marco;Arusha


Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amesema serikali kupitia ofisi ya mkoa wa Arusha inaendelea kuwekeza kwenye miundombinu ya kimkakati na kuhakikisha haiwi kikwazo katika kufanikisha uwekezaji unafanyika nchini.

Mongela ameyasema hayo wakati akifungua Mkutano wa baraza la biashara la Mkoa wa Arusha uliohusisha majadiliano baina ya sekta ya Umma na Sekta binafsi kwa maendeleo endelevu na jumuishi.

Meneja wa Miradi na Maendeleo kutoka katika Taasisi ya TAHA jijini Arusha,Anthony Chamanga katika Mkutano huo amesema kuwa katika kipindi cha Oktoba 2021 hadi mwaka huu,taasisi hiyo imeweza kuuza mazao nje ya nchi takribani tani 2500 yaliyotokana na wakulima wadogo huku akisema kuwa fursa ya masoko katika mkoa wa Arusha ni kubwa zaidi.

Anthony amesema kuwa katika kipindi cha hivi karibuni TAHA imeweza kuleta minyororo ya thamani ya mazao mipya ambayo inazalishwa kwa ajili ya soko la nje.

"Mkoa wa Arusha una uwekezaji mbalimbali uliofanyika kwenye mazao ya horticultural na makampuni baadhi yamewekeza kiasi cha shilingi bilioni 133 ambapo makampuni mengine yanajihusisha na uingizaji wa mazao hayo, yamewekeza zaidi ya bilioni 50 huku wakulima wadogo wakiwekeza kiasi cha fedha kisichopungua milioni 40".alisema Anthony Meneja miradi na maendeleo kutoka TAHA

Ameongeza kuwa Mkoa wa Arusha ni Mkoa ambao umezungukwa na mikoa mbalimbali ambayo hailimi kwa kiasi kikubwa mazao ya horticultural hivyo kuifanya fursa ya masoko katika mkoa wa Arusha kuwa kubwa kwa idadi ya watu milioni 2.3.

"Lakini pia tuna soko kubwa katika mikoa ya Dodoma,Dar es salaam,na nchi jiranj ya Kenya katika miji ya  Nairobi na Mombasa  pamoja na umbali wake ".alisema Anthony

Vilevile ameongeza kuwa katika takwimu za kitaifa TAHA imeweza kupeleka kiasi cha Tan 37240 za mazao ya horticultural nchini Kenya ambapo kiasi hicho kimepitia kwenye minada huku mkoa wa Arusha ukiwa ni sehemu kubwa na muhimu ya kupitisha mazao ya horticultural hivyo kupelekea  mkoa wa Arusha kuweza kuwa wanufaika na fursa hiyo.

Sambamba na hayo ameongeza kuwa suala la mabadiliko ya tabia ya nchi ni suala ambalo linaathiri kwa kiasi kikubwa uzalishaji kutokana na kupungua kwa mvua pamoja na uwepo wa magonjwa ya mimea.

Share To:

Post A Comment: