Naibu Waziri wa Mji ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya Mhandisi Maryprisca Mahundi machi 9,2023 amefanya kikao kazi na watumishi wa sekta ya maji Mkoa wa Mbeya chenye lengo la kuwapongeza na kuwatia moyo kwa namna wanavyokabiliana kuzitatua changamoto za maji Jijini Mbeya na Mbalizi.

Awali Mahundi amepokea taarifa ya hali ya upatikanaji wa maji Jiji la Mbeya na Mji wa Mbalizi taarifa iliyosomwa na Mkurugenzi wa uzalishaji na usambazaji maji Mhandisi Barnabas Konga.

Aidha amepokea taarifa fupi kutoka Chama Cha Wafanyakazi TUGHE iliyosomwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Yassin Msuya.

Katika kikao hicho Mahundi amewapongeza wafanyakazi kila mmoja kwa nafasi yake sambamba na ushirikiano baina yao ili wananchi wapatiwe huduma bora ya maji.

Katika hatua nyingine amewataka watumishi kutobweteka ofisini badala yake watoke kwa wananchi kusikiliza kero zao na kuzitatua huko huko kwa kushirikiana na viongozi wa Mkoa.




Share To:

Post A Comment: