Na John Walter-Manyara

Mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro nyerere amewataka wananchi kushirikiana na serikali na wadau wengine kupinga vitendo vya kikatili vilivyoshamiri katika mkoa huo.

Wito huo ameutoa wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambapo katika mji wa Babati yameadhimishwa leo Machi 13, 2023 katika uwanja wa Kwaraa baada ya siku husika machi 8,2023 kuwepo kwa shughuli nyingine iliyolazimu kusogezwa mbele.  

Makongoro amesema  nguvu Zaidi zinahitajika  katika kupinga ukatili wa kijinsia hususani kwa wanawake, watoto na hata wanaume kwa kuwa nao wanafaniywa  vitendo hivyo.

Takwimu zinaonesha kuwa mkoa wa Manyara unashika nafasi ya kwanza kitaifa kwa vitendo vya kikatili na nafasi ya kwanza kwa vitendo vya ukeketetaji,  huku kwa mwaka 2022  ukishika nafasi ya pili.

Mkuu wa mkoa wa Manyara Charles Makongoro Nyerere anasema takwimu hizo zinautia dosari mkoa.

Nyerere amewataka wananchi kushirikiana na serikali na wadau wengine kupinga vitendo vya kikatili vilivyoshamiri katika mkoa huo.

Kwa upande wake mkuu wa dawati la jinsia polisi mkoa wa Manyara Witnes Kimario, ametoa wito kwa wakina mama kuendelea kuwa wanaharakati wa kupinga ukatili wa kijinsia kwa kuripoti Polisi vitendo hivyo ili hatua zichukuliwe kwa wahusika.

Ameitaka jamii kutoa taarifa hata kama wataona kiashiria cha ukatili na sio kusubiri hadi utekelezwe.

Share To:

Post A Comment: