Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo alipozungumza na wakazi na wanachama wa CCM Shina namba 5, Tawi la Iguguno Kaskazini, Kata ya Iguguno wilaya ya Mkalama.  

Na Dotto Mwaibale, Mkalama 

MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama mkoani Singida James Mkwega amemuomba Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) Daniel Chongolo kuongeza idadi ya walimu ambao hawatoshi wilayani humo.

Mkwega alitoa ombi hilo kwa Chongolo wakati wa siku ya nne ya ziara yake ya kukagua ilani ya chama hicho na kukagua miradi ya maendeleo wakati akizungumza na wananchi wa shina namba tano Kata ya Iguguno Machi 2, 2023.

"Ndugu Katibu Mkuu Rais Samia Suluhu Hassan amefanya kazi kubwa ya kutoa fedha na kujenga madarasa katika halmashauri yetu lakini changamoto kubwa iliyopo hatuna walimu wa kutosha tunaomba ukatuombee hatusaidie katika hilo" alisema Mkwega.

Chongolo akielezea changamoto hiyo alimuhakikishia Mkwega kuwa jambo hilo atalifanyia kazi na kuangalia usawa wa walimu waliopo kati ya mjini na vijijini.

Wakati huohuo Chongolo amesema atakwenda kuwaona wahusika na kuwahakikishia wananchi wa wilaya hiyo kujengwa kwa barabara ya kiwango cha lami kutoka Iguguno hadiimakao makuu ya wilaya ya Mkalama Nduguti.

Aidha Chongolo alisema barabara hiyo haitaishia Nduguti pekee bali itafika hadi Sibiti wilayani humo, Meatu mkoani Shinyanga na kuunganisha mikoa ya Manyara na Arusha.

Chongolo alitoa maelezo hayo kufuatia ombi lililotolewa na Mbunge wa Jimbo la Iramba Mashariki Francis Isack kuomba kujengwa kwa barabara hiyo ya kilometa 42.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Daniel Chongolo aakisalimiana na wananchi na wanaccm baada ya kuwasiliShina namba 5, Tawi la Iguguno Kaskazini, kata ya Iguguno wilaya ya Mkalama kuzungumzana wanachama wa chama hicho.
Vijana wa itifaki wa wilaya ya Mkalama wakionesha umahiri wa kuruka wakati wakimsubiri Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa, Rehema Sombi akizungumzakwenye mkutano huo.
Mbunge wa Iramba Mashariki Isack Francis akizungumza kwenye mkutano huo.

 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Sophia Mjema akizungumza kwenye mkutano huo.

Mwenyekiti wa CCM Mkoawa Singida,Martha Mlata akizungumza kwenye mkutano huo. 

Share To:

dottomwaibale

Post A Comment: