Na Denis Chambi,  Tanga.

MASHIRIKA yote yasiyokuwa ya kiserikali hapa nchini yametakiwa kuendelea kutekeleza wajibu wao katika  kulipa kodi kwa wakati sambamba na kusimamia sheria,  kanuni na taratibu zilizopo katika utendaji kazi kwa kuzingatia maslahi ya taifa.

Wito huo umetolewa  na mwakilishi wa katibu tawala mkoa wa Tanga George Mbaga wakati akifungua semina  iliyoyakutanisha mashirikia binafisi yaliyopo ndani ya mkoa huo ikiandaliwa na shirika la Foundation Civil Society 'FCS' kwa lengo la kuwajengea  uwezo wa kujiendesha , kuzingati sheria miongozo na taratibu za nchi pamoja na kuwakumbusha wajibu wao  katika maendeleo ya Taifa hususan katika kutekelez kwa vitendo sheria ya ulipaji kodi.

"Mashirika yaliyo  mengi yanasema ni mashirika ya huduma kwa hiyo hawana mamlaka ya kulipa kodi lakini ukweli ni kwamba kila shirika limeajiri wa fanya kazi hivyo ukishaajili ni lazima uende katika  sehemu ya ulipaji kodi ni muhimu kwa sababu maendeleo ya nchi yanategemea kodi  hivyo ni lazima wazingatie kuwa wanatekeleza kanuni na miongozo iliyotolewa na serikali" alisema Mbaga

Aidha alisema kuwa licha ya mashirika mengi yaliyopo hapa nchini kutegemea  fedha za wafadhili ili kuweza kujiendesha ni vyema kuzingatia sheria  kanuni na maslahi ya Taifa akiyataka kuwa na miradi ambayo inaweza kuwasadia pamoja na kusimamia malengo yao waliyojiwekea.

"Mashirika mengi yanategemea fedha za wafadhili,  na unapotegemea wafadhili pengine wanapenyeza ajenda ambazo sio sahihi kwa maendeleo ya  na utamaduni wetu  hivyo wengi wakikosa  wanakuwa  hawatekelezi malengo yao hivyo tunasisitiza  taasisi hizi ziwe na miradi endelevu,  ziwe na maengo ya kati na ya  muda mfupi  ambayo yanatekelezeka " alisisitiza.

Pamoja na hayo Mbaga aliyapongeza mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa yakiunga mkono jitihada za serikali za kupiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia vilivyokuwa vikokea katika jamii ambako wamekuwa wakitoa huduma kwa karibu zaidi.

"Kulingana na taarifa za utendaji wa zilizowasilishwa  kwa msajili wa mashirika kwa kipindi cha 2022/2023 mashirika yamechangia kwa kiwango kikubwa  maendeleo hasa katika utekelezaji wa afua za afya,  elimu ukatili wa kijinsia,  msaada wa kisheria uwezeshaji wananchi kiuchumi pamoja na kutoa huduma stahiki kwa makundi maalum wakiwemo wenye ulemavu,  wazee ,  wajane na wanao ishi kwenye mazingira hatarishi" aliongeza Mbaga.

Akizungumza kwa niaba ya  shirika la  Foundation For Civil Society  Nicholaus Mhozya ambaye ni afisa Program mwandamizi alisema kuwa licha ya juhudi mbalimbali wanazoendelea kuzifanya katika kuisaidia serikali ni vyema wakatambua kuwa wana wajibu mkubwa wa kuendelea kulipa kodi  kwa kufuata sheria kanuni na taratibu zinazowaongoza ili kuepuka adhabu ambazo  wanaweza kukumbana nazo ikiwa ni pamoja na kufutiwa usajili.

"Kwa nadharia tu ya kawaida ni kwamba sisi ni mashirika ambayo sio ya kiserikali  hatutengenezi faida za kugawana,  na hata inapotokea tunategeneza faida ni zile ambazo zinarudi kwenye jamii  wengine tumekuwa tukijisahau kwamba kwa sababu tu hatutengenezi faida kwahiyo hatutakiwi kulipa kodi  kumbe sii hivyo inapokuwa ishakuwa tasisi na inajiendesha  kisheria kuna mazingira ambayo yatakulazimu ulipe kodi" 

"Kulipa kodi ni wajibu wa kuweza kuleta maendeleo lakini kuepukana na migogoro ambayo mwisho wa siku  unaweza kuingia kwenye adhabu ambayo itakukatisha tamaa kufanya kazi za jamii" alisema Mkondya.

Mkondya alisema mashirika mengi yamekuwa yakishindwa kusimamia malengo yao waliyojiwekea na kukiuka sheria na taratibu zinazowaongoza hapa nchini hivyo kujikuta wanakiuka taratibu za nchi ambapo mpaka sasa mashirika yapatayo elfu nne yameshafungiwa

"Tunafahamu kuwa katika hii sekta tunafanya kazi  na watu wa aina tofauti na kuanzisha taasisi ni suala la hiari, serikali inatambua kwamba tuna mchango kwenye jamii katika kusukuma maendeleo lakini katika michango yetu haitupi ruhusa ya kujiendesha bila kuzingatia sheria  zilizopo ni vyema kuendelea kuzingati na kutekeleza kaa vitendo ili malengo waliyojiwekea yaweze kutimia, "

Shirika hilo  la Foundatio For Ciliv Society (FCS) lililoanzishwa mwaka 2002  limekuwa ni mwamvuli kwa mashiriki na taasisi mbalimbali zisizokuwa za kiserikali hapa nchini ambapo limekuwa likifanya kazi kwa karibu katika kuyawezesha ruzuku  pamoja na kuyajengea uwezo wa kujiendesha hasa kupitia sheria inayowasimia na kuwaongoza hapa nchini.

Akizungumza mwakilishi  baraza la mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kwa mkoa wa Tanga Miraji Malinda amesema kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa fedha ndani ya mashirika mengi kwaajili kujiendesha akiwaomba viongozi  kuongeza wigo wa ushirikiano baina yao na wadau wengine pamoja na serikali.

"Changamoto ya upatikanaji wa maswala ya fedha umekuwa ni mkubwa kwa upande wa mashirika lakini tuone ni namna gani ya kuweza kuongeza wigo wa kuaminika kwa wafadhili kuongeza ushirikino  na serikali pamoja na wadau mbalimbali" alisema 

"Tunaiomba serikali kuweza kutuunganisha na wadau wengine mfano kupita mashirika ya kibiashara hasa kayika  mpango  mkakati wa uendelevu wa Cooperate Social Responsibility 'CSR' ambayo inatakiwa ije kwetu sisi mashirika ambayo ndio tunafanya kazi kwa karibu sana na jamii" alisema  Malinda.

Foundation Civil for Society limekuwa likijengea uwezo mashirika yote yasiyokuwa ya kiserikali  ambapo hadi sasa limefika katika mikoa kumi ya Tanzania bara wakilenga pia kuifikia mikoa yote nchini kwa lengo la kuhakikisha ustawi ndani ya mashirika hayo unakuwepo ambayo yatachangia katika maendeleo ya Taifa. 

Baadhi ya viongozi wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali mkoa wa Tanga wakiwa wanafatilia semina iliyotolewa na Shirika la Foundation for Civil Society march 23,2023 iliyofanyika  katika ukumbi wa YDCP jijini Tanga

Mwakilishi wa baraza la mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kwa mkoa wa Tanga Miraji Malinda.

Afisa Program kutoka shirika la  Foundation for Civil Societty Nicholaus Mhozyaakizungumza na waandishi wa habari mara baada ya semina waliyoitoa kwa viongozi wa mashirika yasiyo ya kiserikali jijini Tanga kattika kuwajengea  uwezo wa kujiendesha , kuzingati sheria miongozo na taratibu za nchi pamoja na kuwakumbusha wajibu wao  katika maendeleo ya Taifa hususan  kutekeleza kwa vitendo sheria ya ulipaji kodi.

Baadhi ya viongozi wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali mkoa wa Tanga wakiwa wanafatilia semina iliyotolewa na Shirika la Foundation for Civil Society march 23,2023 iliyofanyika  katika ukumbi wa YDCP jijini Tanga
Share To:

Post A Comment: