Mkuu wa kitengo cha Mifugo na Uvuvi halmashauri ya wilaya ya Malinyi Absalom Gepson Mwasumbwe .



Na mwandishi wetu,Malinyi

Jumla ya majosho manne yanatarajiwa kujengwa na halmashauri ya wilaya ya malinyi kwa ajili ya kuogeshea mifugo ambapo wilaya ya Malinyi ni miongoni mwa wilaya nchini znye uhaba wa majosho hayo.

Vijiji vya Malinyi vina idadi kubwa ya wafugaji ambapo ujenzi huo unatajwa kuongeza tija katika ufugaji hasa kipindi hiki ambacho mheshimiwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan ameweka mkazo ujenzi wa majosho katika kila wilaya nchini ambapo February mwaka huu alitoa kiasi cha shilingi bilioni 5.9 ili kujengwa majosho hayo. 

Mkuu wa kitengo cha mifugo na uvuvi halmashauri ya wilaya ya Malinyi bwana Absalom Gepson Mwasumbwe amesema tayari wameshatenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa majosho hayo ambayo ni sehemu karibu na wafugaji wanaoishi katika tarafa za Mtimbira na Ngoheranga.

Amesema wametenge vijiji vinne katika tarafa hizo kwa ajili ya ujenzi wa majosho ambayo yatagharimu kiasi cha shilingi milioni 92 mpaka kukamilika kwake na zitatumika  pia nguvu za wananchi.

Ameainisha kuwa tayari wameshatoa elimu kwa wafugaji kuhusu umuhimu wa uwapo wa majosho katika maeneo ao pamoja na uundwaji wa kamati za pamoja za usimamizi wa ujenzi kwa kila Kijiji.

Amevitaja vijiji ambavyo vinakwenda kunufaika na ujenzi wa majosho hayo ni Kijiji cha Ihowanja kitongoji ch Mwambike,Kijiji cha Tanga,Kijiji Kiswago na Usangule kitongoji cha Mipululu.

Amesema mradi huu utanifaisha jamii ya wafugaji ambao wana upungufu wa majosho ndani ya wilaya ya Malinyi na kusema utekelezaji wake ulipaswa kuwa katika mwaka wa fedha 2021/2022 lakini ulichelewa kulingana na fedha.

Akizungumzia hali ya minada katika halmamshauri hiyo amesema mpaka sasa ipo minada mitano iliyosajiliwa kisheria kwa mujibu wa sharia ya nyama namba 10 ya mwaka 2006 chini ya kanuni ya masoko na mifugo kifungu namba 5.Ambapo kupitia sharia hiyo tayari minada ya Njiwa (itete), Salamiti, Biro,Tanga na Mabanda imesajiliwa kama minada ya upili kwa mujibu wa sharia hiyo na inafanya kazi.

Kulingana na mahitaji wamelazimika kusajili mnada mwingine wa Kilosa kwa mpepo ambao upo katika hatua za usajili kwa mujibu wa sheria na ukikamilika utaanza kazi.

Mfugaji bwana Saulo Mashimba wa kitongoji cha salamiti anasema kulingana na uhaba wa majosho itawasaidia katika kuogesha mifugo na kuondoa tatizo la magonjwa.

Aidha amesema majosho ndiyo msingi wa mifugo kuwa bora ambapo ameishukuru serikali kuanza mkakati wa ujenzi wa majosjo katika vijiji ambavyo vina idadi kubwa ya mifugo.

Bwana Masalo Kajua anasema endapo majosho hayo yatakamilika itawasaidia sana katika ufugaji na hasa wakati huu ambao serikali inasisitiza kufuga kisasa na kwa tija.
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: