Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Malinyi pamoja na baadhi ya wataalam WA halamshauri hiyo wakitembelea maghala ya korosho ya chama kikuu cha ushirika cha TANECU wilayani Tandahimba kwa lengo la kujifunza mfumo wa stakabadhi ghalani Kwa zao la korosho
Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Malinyi pamoja na baadhi ya wataalam WA halamshauri hiyo wakitembelea maghala ya korosho ya chama kikuu cha ushirika cha TANECU wilayani Tandahimba kwa lengo la kujifunza mfumo wa stakabadhi ghalani Kwa zao la korosho

Na wandishi wetu,Tandahimba.


Madiwani wa halmashauri ya Wilaya ya Malinyi wanajifunza mfumo wa stakabadhi ghalani wilayani Tandahimba kwa lengo la kuboresha mfumo wa makusanyo fedha katika mazao yanayolimwa katika wilaya ya Malinyi.


Tandahimba wilaya iliyoanzishwa mwaka 1991 katika mkoa wa Mtwara imefanikiwa pakubwa katika ukusanyaji wa fedha za mazao mbalimbali kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani.

Mazao ambayo yamefanikiwa katika halmashauri hiyo ni korosho na ufuta ambayo pia yanalimwa wilayani malinyi.


Mafunzo hayo ni mahususi kwa ajili ya kufanikisha mfumo wa stakabadhi ghalani ambao katika msimu wa kilimo wa mwaka 2021/2022 ulitumika kuuzia zao la korosho katika chama kikuu cha ushirika cha Ulanga kilombero ambacho ni chama kikuu katika wilaya tatu za Malinyi,Kilombero na Ulanga.


Akizungumza katika mafunzo hayo mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tandahimba mheshimiwa Baisa Baisa amesema mfumo huo wa stakabadhi ghalani ukisimamiwa vema unaweza kusaidia upatikanaji wa mapato makubwa katika halmashauri ambapo wao kupitia mfumo huo wamefanikiwa kukusanya kiasi cha tani 23038.


Huku kiwango cha juu kikiwa tani 74138 msimu wa 2017/18.


Kulingana na hoja hizo ambazo zimetolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Tandahimba baadhi ya madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Malinyi walipata nafasi ya kuuliza maswali akiwemo mheshimiwa Diwani wa kata ya Malinyi mjini mheshimiwa Said Tira ambae alitaka kujua namna ya kukusanya kodi mbalimbali katika zao la korosho ambalo ndilo hasa lililoingizwa katika mfumo huo wilayani Malinyi.


Mwanasheria wa halmashauri ya Tandahimba ndugu Zuberi Salahani akijibu hoja hizo aliwataka madiwani wa halmashauri ya wilaya ya malinyi kuhamasisha wananchi kulima mazao ambayo wanalenga kuyauza katika mfumo wa stakabadhi ghalani.


Ameyataja mazao hayo kuwa ni ufuta na korosho lakini ameshauri halmashauri ya wilaya ya Malinyi kuanza kutengeneza mfumo maalum wa uuzaji zao la mpunga ambalo ndiyo zao kuu la kilimo katika wilaya hiyo.


Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya malinyi Martin Mhode amesema kufikia msimu wa kilimo wa mwaka 2021/2022 halmashauuri hiyo ilifanikiwa kuuza zao la korosho kupitia mfumo wa stakabadhi ghalani na kufanikiwa kuuza Zaidi ya tani 94,000.


Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Malinyi mheshimiwa Lucas Mgomahenga amesema madiwani wa malinyi wapo tayari kuzingatia ushauri na kutengeneza mfumo ambao utawasaidia kukusanya mapato kupitia mazao ambayo yatawekwa katika utaratibu wa stakabadhi ghalani.

MWISHO

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: