Mkuu wa wilaya ya Iringa Veronica kessy akiongea wakati wa maazimisho ya siku ya mwanamke duniani kwa upande wa wilaya hiyo yaliyofanyikia katika Kijiji cha Migori kata ya Migori
Loveness mayingu mkaguzi msaidizi jeshi la polisi kitengo Cha dawati la jinsia  akizungumza na wanawake katika maadhimisho ya siku ya mwanamke katika wilaya ya Iringa ambapo alisema kuwa wanawake kupunguza malumbano na waume zao ili kuondokana na ukatili wa vipigo .
Maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani wilaya ya Iringa yaliyofanyika kata ya migoli tarafa ya Isimani

Na Fredy Mgunda, Iringa.

JUMLA ya matukio ya ukatili 2614 dhidi ya wanawake na watoto Wilaya ya Iringa yametolewa taarifa kwa jeshi la polisi mkoa wa Iringa kutoka mwaka 2019 hadi 2022 huku chanzo kikitajwa kuwa wanawake kubishana na waume katika familia mbele ya watoto.


Hayo yamezungumzwa na Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la polisi Mkoa wa Iringa Loveness Mayengu katika maadhimisho ya siku ya wanawake Wilaya ya Iringa huku akiwaasa wanawake kutokuwa na tabia kubishana na wanaume zao mbele ya watoto


Romana Kinyaga ambaye ni kiongozi wa jukwaa la wanawake kata ya Migori alisema kuwa serikali na wadau wa maendeleo nchini wamehimizwa kuongeza jitihada za kuwafikia wanawake wengi na kuwajengea uwezo wa kuendeleza shughuli za kibunifu walizozianzisha kwa lengo la kujiimarisha kiuchumi

Kinyaga akisoma Risala katika maadhimisho ya siku ya wanamke duniani ngazi ya Halmashauri ya wilaya ya Iringa amesema licha ya jitidaha zilizopo bado kuna kundi kubwa la wanawake halijafikiwa kikamilifu.

Kinyaga  alisema kuwa jitihada zaidi zinahitajika ili kulifikia kundi kubwa zaidi na kuliwezesha kuendana na fursa ya ubunifu na teknolojia ili kufikia usawa wa kijinsia

Kwa upande mkuu wa wilaya ya Iringa na aliyekuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Veronica Kessy alisema kuwa kutokana na uwepo wa matukio ya ukatili kwa wanawake bado kunawanaume waofanyiwa ukatili na hawatoi taarifa hivyo kuwataka kutoona aibu ili kupunguza matukio hayo.

“tunapinga ukatili kwa jinsia zote sana wanawake lakini sasa wimbi kubwa wapo wanaume ambao wanatembezwa kichapo lakini wamekaa kimya na wao wanamakovu yao sasa mwanaume akipata makovu,mwanaume ukifanyiwa ukatili toka nenda kaseme mwanamke vivyo hivyo usione aibu tumia ngazi zote kuanzia wazee wa mila viongozi wa dini yote hiyo ni kutafuta suluhu ili kuondoa makovu yaliyopo mioyoni mwa watu na familia ziishi kwa amani”

Alisema kuwa migogoro ndani ya familia imekuwa ikipelekea wanawake kuachana na ndoa zao na kukimbilia kwa vijana wadogo aliowataja kama “dogodogo” huku tabia hiyo ikiharibu maadili, mila na desturi za jamii yetu.

"Lakini kina mama pia tumeingia kwenye mtindo wa kubaka vijana,unaachana na mume unaenda kutafuta  dogodogo na dogodogo nao wanapenda kulelewa si ndiyo na wao kwa  kuwa wanapenda kulelewa na akiona mama anauwezo wa kakipato kake vijana wanaanza kubweteka acheni vitendo vilivyo kinyume na maadili twende tukajenge kizazi chenye maadili  baba mama tukatekelze wajibu wetu"

Kessy katika hotuma yake amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto zinazowakwamisha mafanikio ya wanawake wilayani humo.

Pamoja na kuwepo kwa maadhimisho hayo mkurugenzi wa wilaya ya Iringa Bashir Mhoja alisema kuwa wamefanikisha kuondoa changamoto za vituo vya afya ambapo wilaya ya Iringa wamejenga zahanati 11 zilizo na huduma zilizoborshwa huku vituo 10 vya afya vikiendelea kujengwa.


Maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani yanaongozwa na kauli mbiu isemayo “UBUNIFU NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA CHACHU KATIKA KULETA USAWA WA KIJINSIA “ ambapo kwa wilaya ya Iringa yamefanyika kata ya Migoli Tarafa ya Isimani  na kutambulishwa kwa kauli mbiu nyingine iliyotolewa na mkuu wa wilaya imayo “SASA BASI UKATILI UMETOSHA".
Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: