Na Joel Maduka,Geita…


Imebainika  Sanaa ya Ubunifu ni moja kati ya ajira ambazo  zikitumiwa vizuri zinaweza kuleta mchango kwa jamii kwani itasaidia vijana wengi kujiajiri na kuongeza kipato chao pamoja na cha familia.


Hayo yamebainishwa na Meneja wa SIDO Mkoani Geita Nina Nchimbi wakati akiwa ni mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Jukwaa  la GOLDEN FASHION FESTIVAL ambalo limefanyika Mkoani Geita,nia ikiwa ni kutambua  na kuibua wabunifu mbali  mbali wa Sanaa ya mavazi na mitindo kutoka mikoa ya kanda ya ziwa.


Amesema wazo la kuanzishwa kwa Jukwaa hilo litasaidia kuwaibua vijana wengi ambao wamekuwa wakijishughulisha na shughuli za ubunifu wa mitindo na mavazi lakini bado awajapata sehemu ya kuonesha shughuli zao.


“Nimpongeza Sanaa mwandaaji wa maonesho haya ya mitindo na mavazi kwani amekuja na kitu kizuri kwenye mkoa wetu wa Geita na pia tunaamini vijana wajitokeza sasa kutoa ushirikiano nia ni wao kutambulika Kimataifa na hapa nchini Kasikana ni Mbunifu wa muda mrefu ambaye ameshiriki Tuzo nyingi hivyo naamini anakwenda kutengeneza ajira mpya kwa vijana”Nina Nchimbi Meneja SIDO Geita.

 

Kwa upande wake muandaaji wa Jukwaa hilo la Sanaa ya ubunifu wa mavazi Bertha Komba alimaarufu Kasikana Collection amesema ameamua kuja na wazo la kuwepo kwa jukwaa hilo kwa lengo la kuibua vipaji vilivyopo Mikoa ya Kanda ya Ziwa.

 


“Tumezoa kuona wabunifu wanapatikana majiji makubwa kama Dar na Arusha lakini sasa tunataka Nchi ijue kuwa na Kanda ya ziwa tunaweza na kunawabunifu wengi ambao bado awajapata majukwa ya kuonesha kazi zao naomba kwa wabunifu wa mavazi na mitindo kanda ya ziwa watumia jukwaa hili kwani ni mali yao”Kasikana Komba mwandaaji wa Jukwaa la Golden Fashion Festival. 

MWISHO…

Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: