Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi ametembelea mtandao wa maji taka na mabwawa saba ya kuhifadhia maji taka yaliyopo Kata ya Kalobe Jijini Mbeya.
Baada ya ukaguzi Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi amefurahishwa na ubunifu na utendaji kazi wa Mkurugenzi mtendaji wa mamlaka maji safi na usafi wa mazingira CPA Gailbert Kayange.
Mahundi amesema Maji haya yakitibiwa yanaweza kurudishwa kwenye mzunguko wa kawaida kwa kuunganishwa kwenye mtandao wa maji safi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira amesema mpaka sasa wana wateja elfu mbili mia tisa sawa na asilimia kumi na tano ya uwezo wa mamlaka na kwamba wanaendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya utunzaji wa mazingira na umuhimu wa kutumia mtandao wa maji taka ambao unasaidia kuhifadhi vyanzo vya maji kwani wananchi wanatumia vyoo vya shimo yale maji hushuka ardhini na kufikia mkondo wa maji hivyo kuwabaribisha uchafuzi wa mazingira.
Aidha Kayange amesema watashirikiana na Jiji kuhakikisha wananchi wote wanatumia mtandao wa maji taka na kushauri wananchi wasiojiunga na mfumo wa maji taka watozwe faini kubwa.
Kayange amesema baadhi ya changamoto kubwa ni wananchi kutumia taka ngumu kwenye mtandao wa maji taka na kila mwaka huongeza kilometa tano na wanatajia kuendelea kupanua mradi.
Katika kutoa hamasa kwa wananchi kujiunga na mfumo wa maji taka mamlaka inatoa motisha wa mabomba sita yenye urefu wa mita sita kila moja lengo likiwa ni kuwapunguzia gharama wananchi ili waondokane na matumizi ya vyoo vya shimo.
Wananchi wakipata elimu hii watasaidia kutunza mazingira sambamba na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira kuongeza mapato yake ambayo yataongeza miradi nyingine.
Post A Comment: