Na;Elizabeth Paulo,Dodoma


Naibu waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe Pauline Gekul amevitaka vyombo vya habari kuhakikisha vinatoa habari zinazokidhi maadili ya mila na Destuli ya kitanzania ili kuhakikisha Jamii ya kitanzania inaelimika kwa maadili ambayo kwa kizazi cha Sasa kumekuwa na mmomonyoko wa maadili.


Mhe Gekul Ametoa kauli hiyo wakati akifunga Mkutano Mkuu wa Mwaka wa watoa huduma wa sekta ya utangazaji Tanzania ulio fanyika kwa Siku mbili katika ukumbini wa Jakaya Kikwete convention center Jijini Dodoma


“Ukiangalia Jamii ya kizazi Chetu cha Sasa kimekuwa na mmomonyoko mkuwa wa maadili kufuatia matukio mbalimbali yanayoendelea hapa nchini kama ubakaji,ukatili wa kijinsia,ulawiti,ushoga na kusagana na mavazi yasiyo na stara haya yote yanatendeka kwa kukosa maadili na momonyoko wa tabia mbaya jambo linalo peleka Jamii yetu kuacha mila na destuli zetu alizo tuachia mhasisi wa Taifa hili hayati Baba wa Taifa Mel Juliasi Nyerere”Amesema Naibu waziri Mhe Gekul


“Sasa niwaagize wamiliki wa vyombo vya habari na Waandishi kuhakikisha kalamu zenu na vyombo vyenu mnajikita kutangaza na kuelimisha kwa sote kupaza sauti kupinga vita hii ya matukio haya kwa kutoa elimu,vipindi mbalimbali na makala nzuri Juu ya kujenga maadili ya kitanzania Ili kuweza kunusuru kizazi hichi”Amesisitiza Mhe Pauline Gekul.Naibu waziri waziri Amesema vyombo vya habari vina nafasi kubwa Sana ya kutangaza na kuelimisha Wananchi kuhakikisha wanafuata maadili ya kitanzania hapa nchi na kuwa na kizazi ambacho kinafuata maadili nawsheria zetu za nchi.


Kwa Upande wake Mkulugenzi wa TCRA Amesema baada ya Mkutano huu kila chombo na Mwandishi anaeajibu wa kutekeleza maadi ya chombo cha habari na kuisaidia serikalini kuhakikisha wanatangaza vipindi,makala na kutangaza habari zenye lengo chanya kwa watanzania kwa kuzingatia maadi na sheria mbalimbali za nchi.
Dkt Jabir Bakari amesema Mkutano huu utaleta mabadiliko makubwa kwa vyombo vya habari na Waandishi wa Habari katika kutekeleza majukumu yao ya kazi za kila siku na TCRA itaendelea kusimamia sheria na maadili kwa vyombo vya habari vitakavyokuwa vikikiuka kanuni,sheria na miongozo vitachukuliwa hatua.


Aidha Dkt Jabir Bakari amesema TCRA imejipanga kuendelea kutoa Elimu kwa vyombo vyote vya habari na kuendelea kuwatembelea katika vituo vyao ili kuweza kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazowakabili na kuweza kuishirikisha wizara ya Habari Mawasiliano na tekinoloji ya Habari ili kuweza kuzipatia ufumbuzi wa haraka .Mkutano huo Mkuu wa mwaka wa watoa huduma wa sekta ya utangazaji nchini umeshirikisha vyombo vya habari mbalimbali kama TV, Redio,One line blog tv ambao umefanyika kwa muda wa siku Mbili Katika ukumbi wa Jakaya Kikwete convention center Jijini Dodoma.

Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: