Na;Elizabeth Paulo,Dodoma

Ili kukidhi mahitaji ya wataalamu wazawa wenye weledi katika vyombo vya usafiri kwa njia maji Chuo Cha Bahari Dar es salaam (DMI) kinaendelea kutoa elimu na mafunzo ya ubaharia kuanzia madaraja ya usaidizi hadi madaraja ya juu ya maofisa wa melini kwa upande wa uongozaji meli au unahodha na uhandisi mitambo ya meli.


Kaimu Mkuu wa Chuo cha Bahari Dar es salama Dkt Tumaini S. Gumuro amesema hayo leo alipokua akieleza utekelezaji wa majukumu ya chuo hicho na kusema chuo kilianzishwa mwaka 1978 na chuo hicho kuwa chuo cha kwanza katika ya vyuo vinne Barani Afrika Mashariki.


Chuo hicho Kimeanzishwa mara baada ya nchi kuwa na uhitaji wa mabaharia ambapo baada ya nchi kupata uhuru mwaka 1961 kulikua na mabaharia wachache na wengi wao walikua ni mabaharia wa ngazi za kuanzia hivyo (DMI) ilianzishwa kama kitengo cha mafunzo ya ubaharia kwa Watanzania.


Aidha amesema kuwa DMI imeanza utaratibu wa kujenga uhusiano na wamiliki wa meli ili kupata nafasi za ajira na mafunzo kwa vitendo kwa ajili ya mabaharia wa kitanzania nje na ndani ya nchi.


“Tayari DMI imefanikiwa kuwaunganisha na waajiri mabaharia 27 na kufanikiwa kupata ajira na mafunzo kwa vitendo,”amesema Dkt.Gurumo.


Pamoja na hayo Dkt.Gurumo ameeleza kuwa Serikali ya awamu ya sita imewezesha kupata maeneo mbalimbali ya kujenga matawi ya DMI katika Mikoa ya Lindi na Mwanza.


“Matawi haya yatakapo kamilika huduma ya elimu na mafunzo ya usalama wa vyombo vya usafiri na usafirishaji kwa njia ya maji itakuwa imesogezwa karibu zaidi na wananchi,”amesema na kuongeza


“Hivi leo mabaharia wapatao 8,700 Walioaajiliwa Tanzania Bara na Tanzania visiwani wanaofanya kazi ndani na nje ya nchi.”


Aidha amesema (DMI) imefanya jitihafa mbalimbali na kupewa hadhi ya kituo cha ubora cha elimu na mafunzo ya ubaharia katika Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya kufanyiwa ukaguzi kupitia Sekretariet ya Umuiya ya Afrika Mashariki.


Kadhalika amesema mipango mengine ya chuo hicho kuwa ni pamoja na kujenga vyombo vidogo vidogo vya usafiri majini ikiwa ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo, Kujenga miundombinu ya chuo kwa viwango vya juu mkabala na ufukwe wa bahari ya Hindi jijini Dar es salaam ilikukidhi mahitaji ya ongezeko la wanafunzi,waalimu na kozi.


Pia wameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwapatia kiasi cha shilingi bilioni 6.5 kwaajili ya kununua vifaa vya kisasa vya kufundishia.


Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: