Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka akiwasilisha Taarifa ya Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi  Chama cha Mapinduzi 2020/2025 kwa kipindi cha miaka miwili.

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Deo Sanga Akizungumza na wanachama wa CCM wakati wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya CCM Mkoa wa Njombe.
Mawaziri, wabunge na Madiwani wa CCM Mkoa wa Njombe wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wakiwa wamepiga magoti wakimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutekeleza miradi mingi ya maendeleo katika Mkoa wa Njombe.
Katibu wa CCM Mkoa wa Njombe Julius Peter akiteta jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Pindi Chana sambamba na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi Afya Festo Dugange.

Na Imma Msumba, Njombe

Mkoa wa Njombe umeendelea na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM kwakuendelea na ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika mkoa huo.

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Antony Mtaka amebainisha Utekelezaji wa miradi hiyo  katika taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya mwaka 2020-2025 kwa Mkoa wa Njombe  katika kipindi cha mwaka mmoja Julai 2021 Hadi Disemba 2022.

Mtaka amesema Mkoa wa Njombe unaendelea kutekeleza mipango ya maendeleo kwa kuzingatia Ilani ya Chama ambapo Dira ya Taifa ya maendeleo 2025 na malengo ya maendeleo endelevu ya Milenia yenye lengo na nia ya kuendelea  kuwatumikia wananchi na kuboresha maisha ya wananchi wote.

Mtaka amesema kama ilani ya chama tawala inavyoelekeza,Mkoa umekusudia kusimamia na  kuelekeza rasilimali zake katika kuimarisha upatikanaji wa huduma bora za Afya,Elimu,Maji,Umeme na Makazi vijijini na Mijini pamoja na kuleta mageuzi ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi katika kujitegema kwa chakula wakati wote na kuchangia kikamilifu kwa maendeleo ya kiuchumi.
 
Amesema serikali ya Mkoa itajikita katika mambo matatu muhimu yatakayogusa maisha ya wananchi ikiwa ni Pamoja na Kusikiliza na kutatua kero za wananchi, kufuatilia wanafunzi ambao bado hawajaripoti mashuleni ambapo amesema asilimia 90 ya wanafunzi kidato cha kwanza wameripoti katika shule mbalimbali ambapo awali ilikua asilimia12.

Aidha Mkoa umeanzisha mkakati wa kuwaondoa wanufaikawa Tasaf baadaya Miaka mitatu Hadi miaka mitano kwa kuanza na Halmashauri ya Makambako ambapo katika ziara ya Waziri Mbashe mwenye dhamana ya  Wizara ya kilimo alitoa miche ya parachichi  elfu 20 yenye thamani ya shilingi millioni Mia moja kwa wanufaika wa Tasaf hao ambapo kila kaya imepewa miche 10.

kutokana na kero kubwa na Changamoto inayowakabili wananchi na wakazi wa mkoa huo  kutozwa ushuru mara mbili kuingia stand kuu Mtaka metoa wito kwa viongozi na wakusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri kutafuta vyanzo vya mapato na kuacha mapato kero kwa wananchi.

Awali akizungumza Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Njombe  Ameupongeza uongozi wa chama tawala chini ya Mwenyekiti wake Dkt Samia Suluh Hasan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutenga fedha nyingi za ujenzi wa miradi ya maendeleo katika mkoa wa Njombe. 

Katika kuwainua kiuchumi halmashauri ya Mkoa  imeendelea kutoa mikopo kwa Vikundi vya akina mama, Vijana  na watu wenye ulemavu ambapo jumla ya shilingi
bilioni 10,660,317,310 zimekopeshwa kwa ambapo vikundi vya wanawake ni 382 vyenye wanufaika 4,062, Vijana vikundi 237 vyenye wanufaika  1,564 pamoja na watu wenye ulemavu kwa vikundi 72 vyenye wanufaika 207.

Maadhimisho ya Miaka 46 ya kuzaliwa kwa Chama cha mapinduzi kwa Mkoa wa Njombe imehudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Chama, Akiwemo Mwenyekiti wa (CCM) mkoa wa Njombe Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Pindi Chana, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi anayeshughulikia Elimu na Afya Dkt. Festo John Dugange, Wabunge, wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi,  Wakuu wa Wilaya, pamoja na wananchi wa Mkoa huo.Share To:

Post A Comment: