Na;Elizabeth Paulo, Dodoma

Vijana Mkoani Dodoma wametakiwa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa mbalimbali za kihalifu na wahalifu pale inapoonekana viashiria vya uvunjifu wa sheria.

Ili kuunga mkono juhudi mbalimbali zinazoendelezwa na jeshi la polisi kupitia miradi mbalimbali ya michezo Mkoa wa Dodoma Uhalifu utapungua hata kumalizia kabisa hivyo Vijana wametakiwa kushiriki katika michezo hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Rosemary Senyamule alitoa wito huo hivi karibuni alipokua alizindua mashindano ya (Polisi Jamii Cup) na kusema mradi huo utaisaidia jeshi la polisi kutanzua matatizo ya kihalifu.

“Mashindano haya yanazinduliwa hapa Dodoma na kufuatiwa na mashindano mengine nchini ambapo dhana hii inaiwezesha Jeshi la polisi na Wananchi kiujumla kushiriki moja kwa moja katika suala zima la kutanzua migogoro mbalimbali kuanzia ngazi ya familia,Mtaa,Kata,Tarafa,Wilaya mpaka Taifa ”.Alisema Senyamule

Katika kuboresha ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na Jamii ipo miradi mbalimbali ikiwemo mashindano ya (Polisi Jamii Cup), Mradi wa Polisi Kata kama miongoni kwa miradi mengine.

Senyamule alisema mradi wa Polisi Kata umewezesha kuwa na mkaguzi wa kila Kata ambao ni wataalamu wa masuala ya Ulinzi na Usalama kwa lengo la kuwafikishia wananchi huduma za ki polisi moja kwa moja kuanzia ngazi ya Kata.

"Kupitia Mradi huu wakaguzi wa Kata wataweza kutatua migogoro mbalimbali ya kifamilia,Kubaini na Kuzuia Uhalifu/Wahalifu sanjari na Kuzuia vitendo vya kikatili na unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto.

Aidha Mkuu huyo wa Mkoa alitoa wito kwa Viongozi wa serikali za mitaa,Vijiji kuwapokea na kuwapa ushirikiano wakaguzi hao kuhakikisha malengo waliyoletewa kwenye Kata yanafanikiwa na kwamba wapo kwaajili ya kuwahudumia wananchi.

“Na hapa nitoe maelekezo Polisi Kata kufanya vikao vya Usalama vya Kata na kutoa elimu kwa wananchi kupitia mikutano ya Vijiji na Vitongoji ili kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kutunza usalama, Amani ya maeneo yao na Taifa nzima, Kuwepo kwenu kule kuwe ni chachu kubwa ya kupunguza na kuondoa matukuo ya Uhalifu.”Alisisitiza Senyamule

Kadhalika alitoa onyo na kuwasihi vijana wasiobadilika ambao wanaendelea na vitendo vya kihalifu kwamba Serikali inatumia mbinu nyingi kwaajili ya kuhakikisha Vijana wanapata Ajira, Kujiajiri, na kujifanyia shughuli mbalimbali za kuwawezesha kupata uchumi.

“Niendelee kutoa wito Vijana badala ya kufanya mambo ya Uhalifu jishughulisheni na kazi halali, Twende kwa watendaji wa kata, wapo Maafisa Maendeleo ya Jamii, zipo Ofisi za Halmashauri ili muweze kufanya shughuli halali za kuwapatia kipato badala ya kufanya matukio ya kihalifu”.Alisema

Na kuongeza “Na kwa wale ambao hawatataka kuacha Uhalifu na wasiotaka kubadilika kupitia miradi yote hii iliyoanziashwa na Jeshi la Polisi na Sera nzuri za nchi yetu wajue kuwa hatua zitachukuliwa kwa wale ambao wanataka wawe mbele ya sheria kwahiyo tuendelee kuhakikisha wale Vijana wachache ambao wanaendelea na Uhalifu tunawadhibiti na nchi yetu ibaki kuwa nchi ya Amani na Utulivu.

Awali akizungumza Mkuu wa Polisi Jamii Nchini Kamishna Faustine Shilogile alisema kuwepo kwa mashindano hayo ni utekelezaji wa moja ya miradi iliyopo ya Polisi Jamii ambapo mradi wa michezo kwa vijana katika Kuzuia na kupambana na Uhalifu una lengo la kutoa elimu ya Usalama kwa Vijana na kuwahamasisha kuondokana na vitendo hasi yanayochangia kufanya vitendo vya Uhalifu,Vurugu ikiwemo Utumiaji wa Dawa za kulevya,Unywaji wa pombe  kupindukia,  Ubakaji,Uwizi, Pamoja na Matendo mengine ambayo yanaenda kinyume na Maadili ya Taifa.


“Pamoja na mradi huu ipo miradi mingine ambayo ilibuniwa na jeshi la polisi ikiwa na lengo la kuishirikisha jamii katika kubaini na Kuzuia Uhalifu ikiwa ni pamoja na mradi wa Polisi Kata,Mradi wa Ulinzi Shirikishi, Polisi na watoto yaani Usalama wetu kwanza, Huduma Bora kwa mteja, Utii Sheria bila Shuruti, Utunzaji wa Mazingira, Utalii Salama,Kilimo na Ufugaji,Kuzuia unyanyasaji wa kijinsi,Kuzuia na Kupambana na Rushwa, Makazi Salama, Na Mradi wa Ulinzi Jirani ”.Alifafanua Shigolile

Akizungumzia Mradi wa Polisi Kata Shilogile alisema kwa Mkoa wa Dodoma wenye Kata 208 tayari askari wapo wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali kwa lengo la kuanzia kwa wananchi kupitia wakaguzi Kata kushirikina na watendaji Kata pamoja na viongozi wengine ndani ya Kata hizo kuhakikisha Uhalifu unazuiliwa kabla Haujatokea. Aidha pamoja na Michezo hii kutumia kama nyenzo muhimu katika kupambana dhidi ya uhalifu,lakini pia wataalamu wanasisitiza umuhimu wa michezo kwani huimarisha ushirikiano na kuleta burudani.

Kwa upande wake Mdhamini wa Mashindano hayo ya Polisi Jamii Cup ametoa Rai kwa Watanzania na wadau mbalimbali kushirikina na Jeshi la Polisi katika shughuli za kijamii za kuijenga taifa na hata katika shughuli zingine.


BAADHI YA PICHA KATIKA UZINDUZI WA MASHINDANO YA POLISI JAMII CUP


PICHA na Benedict Mlawa wa Jeshi la Polisi 
Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: