Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo (pichani) kesho Februari 27, 2023,anatarajia kuanza ziara ya kikazi ya siku sita katika Mkoa wa Singida kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwenye halmashauri sita za mkoa huu kuona kama ilani ya CCM inatekelezwa vyema.

Na Dotto Mwaibale, Singida 

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Daniel Chongolo,anatarajia kuanza ziara ya siku sita kesho (Februari 28) katika Mkoa wa Singida kwa ajili ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwenye halmashauri sita za mkoa huu kuona kama ilani inatekelezwa vyema.

Katibu Mwenyezi wa CCM Mkoa wa Singida, Ahmed Kaburu, akizungumza na waandishi  wa habari leo Februari 27, 2023 alisema katika ziara hiyo Chongolo ataambatana na  viongozi wa sekretarieti ya chama hicho taifa, ataanzia ziara katika Wilaya ya Manyoni.

Alisema akiwa katika Wilaya ya Manyoni atatembelea na kukagua mradi wa maji Kintiku Lusilile, ujenzi wa sekondari ya wasichana Solya, ujenzi wa barabara ya Itigi-Rungwa,sekondari ya Itigi na kutembelea miradi ya chama na kuzungumza na wananchi.

Februari 28, mwaka huu, Chongolo atakuwa katika Wilaya ya Ikungi ambako atatembelea Chuo cha Ufundi Stadi VETA,ujenzi wa migodi wa Shanta Mining Limited, Hospitali ya Wilaya ya Ikungi,kufungua jengo la ofisi ya CCM wilaya na kuzungumza na wananchi.

Katika Wilaya ya Iramba ambako atakuwa Machi 1, atatembelea zahanati ya Kinambue, Hospitali ya Wilaya, sekondari ya Lulumba,mradi wa maji Kiomboi na kuzungumza na wananchi.

Chongolo atatembelea Wilaya ya Mkalama Machi 2, atatembelea sekondari ya Iguguno,kituo cha afya Kinyangiri, hospitali ya Wilaya ya Mkalamba,kutembelea ujenzi wa kituo cha polisi kuhudhuria mkutano wa shina Iguguno.

Wilaya ya Singida Vijijini atatembelea shule ya Sekondari Mtinko, Hospitali ya Wilaya Ilongero,Kituo cha Afya Ngimo, Zahanati ya Pohama,Shule ya Sekondari Mwanamwema na kuzungumza na wananchi.

Chongolo atahitimisha ziara yake Machi 4 ,katika Wilaya ya Singida mjini ambako atatembelea mradi wa CCM mkoa, Hospitali ya Rufaa, atatembelea wajasiriamali wa soko kuu la Singida,Jengo la Mama na mtoto kituo cha Afya Sokoine, kutembelea Mwenge Sekondari na kiwanda cha kukamua alizeti cha Shulu na kuzungumza na wananchi.

dottomwaibale

Post A Comment: