Afisa maendeleo ya jamii Halmashauri ya wilaya ya Iringa Saumu kweka akiongea na wanufaika wa mikopo hiyo asilimia 10 ya mapato ya ndani

Afisa maendeleo ya jamii Halmashauri ya wilaya ya Iringa Saumu kweka kwenye picha ya pamoja na wanufaika wa mikopo hiyo asilimia 10 ya mapato ya ndani
Afisa maendeleo ya jamii Halmashauri ya wilaya ya Iringa Saumu kweka akiongea na wanufaika wa mikopo hiyo asilimia 10 ya mapato ya ndani

Na Fredy Mgunda, Iringa.


Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imekabidhi hundi ya kiasi shilingi 247.9 za mkopo Kwa vikundi vya wajasiriamali ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Serikali katika kuwasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi.

Akikabidhi Hundi hiyo Kwa vikundi Kutoka vijiji mbalimbali Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Saumu Kweka alisema Fedha hizo ni muendelezo wa mikopo inayotolewa na Halmashauri hiyo.

Kweka ambaye ni Mkuu wa Idara ya maendeleo ya Jamii katika Halmashauri hiyo alifafanua Kuwa  vikundi vya wanawake 18 wamekabidhi mkopo wa kiasi shilingi milioni 96 na Laki 6, Vijana vikundi 19 wamepata milioni 112 Laki 6, pamoja na vya Watu watu wenye Ulemavu vipatavyo 19 wamepata mkopo wa shilingi million 38 na Laki saba.

Akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji katika Hafla hiyo Saum Kweka alivitaka vikundi hivyo kuhakikisha Fedha walizopatiwa wanazielekeza katika miradi waliyokusudia Huku akisiisitiza kurejeshwa Kwa wakati mkopo wa Fedha walizopatiwa Ili kusaidia vikundi vingine pia kunufaika na Fedha hizo zinazotokana na mapato ya ndani.

"Tena Niviombe vikundi ambavyo havijapata mikopo katika awamu hii kuendelea Kuwa wavumilivu na warejee kujaza fomu za mkopo Ili kujiweka tayari Kwa awamu ijayo" Alisema Kaimu Mkurugenzi Saumu Kweka.


Kwa upande wake Mkuu wa kitengo Cha Mawasiliano Serikalini Halmashauri ya Wilaya ya Iringa Zaitun Omary amewakumbusha wanufaika wa Fedha hizo za mkopo kutambua kuwa Serikali haitosita kuchukua hatua ikiwemo kuvifungulia mashtaka vikundi vitakavyokaidi urejeshaji wa mikopo Kwa wakati.

Zaituni alivitaka vikundi Hivyo kutambua Kuwa fedha wanazopata siyo hisani Bali ni za mkopo Hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanazirejesha Kwa wakati Kwa Ili kuiwezeaha Halmashauri hiyo ni kuendelea kutoa mikopo Zaidi Kwa vikundi vilivyokosa fursa Kwa awamu hii.


Mwisho


Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: