Na; Elizabeth Paulo,Dodoma

Mamlaka ya Serikali Mtandao (e GA) kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha Na Mipango imefanikiwa kuunda mfumo wa Ukusanyaji wa Malipo ya Serikali kielektroniki (GePG) kwa lengo la kuimarisha uwazi na udhibiti katika Ukusanyaji wa mapato ya Serikali.


Kupitia mfumo huo Serikali inao uwezo wa kufahamu mapato yanayoingia kila siku ambapo mpaka sasa Taasisi na Vituo vya kutolea huduma 948 zinatumia mfumo huo.


Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Serikali Mtandao (e GA) Mhandisi Benedict B. Ndomba ameyasema hayo leo jijini Dodoma alipokua akielezea Utekelezaji wa Majukumu ya Mamlaka mbele ya waandishi wa Habari.


"Mfumo huu unaisaidia Serikali kuwa na Uoni wa mapato yake sasa hivi mtu yeyote mwenye Mamlaka ya kuona makusanyo anaweza akaona tangu asubuhi mpaka jioni mapato yapo kwa kiasi gani na Taasisi ipi imekua na makusanyo mengi."Alisema Ndomba


Ndomba amesema Mamlaka imeendelea kutekeleza majukumu yake kwa kuzingatia misingi yake sita ikiwemo Uadilifu, Ubunifu, Kuthamini wateja, Kufanya kazi kwa pamoja, Ushirikiano na Weledi.


Mhandisi huyo ametoa Wito kwa Taasisi za umama ambazo hazijaunganisha mfumo wa Ubadilishaji Taarifa Serikalini (GovESB) kuunganisha ili ziweze kuibadilishana taarifa na Taasisi nyingine pale inapohitajika.



"Mfumo huu umewezesha mifumo mbalimbali ya Serikali kuwasiliana na kuibadilishana taarifa na Taasisi zaidi ya 50 zimewezeshwa mifumo yake kuibadilishana taarifa kupitia mfumo huu hivyo nisisitize kwa Taasisi ambazo hazijajiunga kujiunga kwa Umuhimu wa Mfumo."Alisisitiza Ndomba


Serikali kupitia Mamlaka ya Serikali Mtandao (e GA) imesaidia upatikanaji wa huduma nyingi za Serikali kwa haraka na mahali popote na Mamlaka kuendelea kutekeleza azma ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha ujenzi wa Serikali ya Kidijiti.



"katika kuhakikisha tunaijenga Serikali ya kidijiti, katika miaka 10 ijayo Mamlaka itaandaa na kutekeleza mikakati madhubuti ili kuimarisha zaidi utekelezaji wa jitihada za Serikali Mtandao kwa kuwa na sehemu Moja ambayo huduma mitandao zote zitakua zinapatikana, Uwezo wa kutumia teknolojia mpya zinazoibuka hasa zile za akili bandika, Sarafu za Kidijiti na teknolojia za kifedha ili kuwesha maboresho ya kiutendaji katika Taasisi za umma na utoaji wa huduma kwa umma."Alisema


Na kuongeza "Mamlaka pia itaandaa vijana wa kitamzania wenye uwezo mkubwa wa Ubunifu katika utekelezaji wa jitihada za Serikali Mtandao, Uzalishaji wa vifaa na miundombinu ya TEHAMA (Hardware) ndani ya Tanzania, Mifumo na Miundombinu ya Serikali Mtandao iliyobora na imara zaidi."


Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa amesema kama Serikali wamenufaika na mfumo wa GePG kwa kudhibiti uvujaji wa mapato ya Serikali.



"Nasema hivi kwasababu kipindi kile cha kukusanya kwa njia ya vitabu Kuna wengine walikua wanavitabu vyao pembeni kwa hiyo fedha unatoa unapewa risiti kumbe risiti hiyo siyo ya Serikali niyakwake mwenyewe na fedha zile haziingii kwenye mfuko kuu wa Serikali kwa hiyo maeneo mengi tumeshapeleka hizo mashine sasa kila ukitaka kulipa unaambiwa lipa kwa control number na hiyo Hela haiwezi kuibiwa na mtu yeyote inaenda Moja kwa Moja kwenye mfuko wa Serikali."Alisema Msigwa


Serikali Mtandao ni matumuzi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ( TEHAMA) katika utendaji kazi wa Taasisi za umma na utoaji huduma kwa wananchi kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utendaji kazi katika taasisi za umma pamoja na kuboresha utoaji wa huduma kwa umma ili huduma hizo zipatikane kwa urahisi, haraka na kwa gharama nafuu kupitia TEHAMA.


Mamlaka imekua ikitekeleza jitihada mbalimbali za Serikali Mtandao katika taasisi za umma tangu kuanzishwa kwake mwaka 2012 ambapo awali Taasisi ilijulikana kama Wakala ya Serikali Mtandao na baada ya kutungwa kwa sheria ya Serikali Mtandao no.10 ya mwaka 2019,ilipewa hadhi ya Mamlaka.



Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: