Mkuu wa wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro Shaka Hamdu Shaka amekemea baadhi ya watumishi ambao wamekua sio waadilifu Kwa kuendekeza rushwa Jambo ambalo linachangia Kuongezeka kwa migogoro ya ardhi wilayani humo.


DC Shaka ameyasema hayo katika baraza la madiwani wilayani humo ambapo amesema  baadhi ya watendaji wa Vijiji na kata ,madiwani na Watumishi wengine  ambao wamekua kikwanzo cha Serikali kukomesha changamoto hiyo Kwa kuchukua rushwa Kwa wafugaji na wakulima wahalifu.


DC Shaka anasema  katika uongozi wake hatakubali kumvumilia kiongozi ambaye atakua Chanzo cha migogoro Kwa kuendekeza rushwa na kuahidi kuwashughulikia Kwa mtu yeyote atakayebainika.


Anasema kwa kipindi kifupi alichokua Kilosa malalamiko mengi yanayoletwa na wananchi yanababishwa na kukosekana Kwa uadilifu Kwa viongozi Jambo ambalo ni kinyume na taratibu za kimaadili.


"nimekaa muda mfupi wa wiki MBili hapa Kilosa nimegundua migogoro ya ardhi inasababishwa na viongozi kukosa uadilifu na uzalendo Kwa kuendekeza vitendo vya rushwa Hivyo sitamvumilia Mtendaji atakayekua  kikwanzo "DC SHAKA



Aidha Shaka amewataka watendaji kubuni vyanzo vya mapato pamoja usimamizi Bora wa ukusanyaji  huku akikemea Matumizi holela ya fedha mbichi na kutaka fedha zote ziingizwe banki ndipo zipaangiwe Matumizi.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza la madiwani halmashuri wilaya ya Kilosa Wilfred Sumari  anasema kinachoendelea ni uzembe Kwani tayari Serikali ya wilaya ilishatoa maekekezo Kila kijiji kufanyike utambuzi wa mifugo na wafugaji , kuunda kamati za usuluhishi ,na kuondoa mifugo ambayo imeingia bila kibali  lakin baadhi viongozi wa kata wamekaidi maagizo hayo na kushindwa Kutekeleza

Sumari anasema  ni muda muafaka sasa Kwa watumishi kuanza kuchukuliwa hatua Kwani ndio wamekua Chanzo za changamoto hiyo Kwa kushindwa Kutekeleza maagizo ya Viongozi wa juu na kusababisha wilaya hiyo kuendelea kuwepo Kwa migogoro.




Share To:

mwangaza wa hbari

Post A Comment: