Na;Elizabeth Paulo,Dodoma

Kaimu Meneja Mpango wa Taifa wa Kifua Kikuu na Ukoma Dkt. Peter Neema amesema pamoja na jitihada zinazofanywa na Serikali kupitia Wizara ya Afya kufikia asilimia 55% za Kupunguza Ugonjwa wa Kifua Kikuu nchini bado kumekuwa na changamoto kwenye uibuawa maambukizi mapya ya Kifua Kikuu ,kutokana wagonjwa wengi kukosa elimu bora juu ya Uibuaji wa gonjwa Hilo.


Dkt. Peter amesema hayo Jijini Dodoma katika Uzinduzi wa Mapitio ya Muhula wa Kati wa Mpango Mkakati wa Taifa Chini ya Awamu ya Sita Na Kusema wanafanya Mkakati wa kuongeza Mashine,Maabara na kutoa elimu kwa Ajili ya kupima Vina Saba vya Kifua Kikuu ili kufikia lengo la Uibuaji wa Ugonjwa huo.


Amesema takwimu zinaonesha kuwa maambulizi mapya yamepungua kwa asilimia 32% kati ya 75% zilizolengwa kufikiwa ifikapo 2025 ili kupunguza Vifo vitokanavyo na Ugonjwa huo.




''Sasa hivi tunategemea kufanyia maboreshi katika mpango mkakati wetu wa sita ili kuchukua reccomendation zilizotolewa katika ripoti ili tuweze kufikia malengo yetu vizuri utakapofika mwisho wa mpango mkakati huu 2025''Dkt Peter




Kwa Upande wake Radia Abeid Khaji Mwakilishi wa Shirika la Shidefa Plus Kutoka Mkoani Shinyanga amesema wanatumia wahudumu wa Afya ngazi ya Jamii kwenda kutoa Elimu Juu ya Kifua Kikuu pamoja na kufanya uchunguzi wa awali kwa wachimbaji wa Madini wenye dalili za Ugonjwa huo ili kupelekwa kufanyiwa uchunguzi zaidi katika vituo vya Afya .




Share To:

ELIZA DOM

Post A Comment: