IMG-20230123-WA0171


OR-TAMISEMI

Naibu Waziri Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Dkt. Festo J. Dugange (Mb) amesema kufikia Januari 2023, Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imeingia mikataba 1,670 yenye thamani ya Shilingi 552,284,112,421.73 sawa na asilimia 95 ya zabuni zote kwa mwaka fedha 2022/23 na kazi zinaendelea kutekelezwa.

Ameeleza hayo Januari 23, 2023 wakati akitoa ya taarifa ya Ofisi ya Rais TAMISEMI kuhusu maazimio ya Bunge yatokanayo na Taarifa ya mwaka ya shughuli za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala Bora na Serikali za mitaa (USEMI).


Amesema zabuni zilizosalia ni 82 na mikataba yake itasainiwa muda wowote kuanzia sasa kabla ya mwezi februari 2022 na Ofisi ya Rais TAMISEMI itaendelea kufuatilia ili kuhakikisha kuwa kazi za zinaanza kwa wakati.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya USEMI iliitaka TARURA isimamiwe kuhakikisha kuwa mikataba ya wakandarasi inatekelezwa kwa wakati ambapo Serikali imelifanyia kazi azimio hilo ambalo asilimia sitini (60%) ya bajeti hutangazwa mara tu bajeti ya Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuidhinishwa na Bunge.


Dkt. Dugange amesema Serikali ilifanya maamuzi makubwa yaliiyoridhiwa na Bunge ya kuiongezea TARURA fedha kwa ajili ya matengenezo, ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya barabara.

Aidha, Dkt. Dugange amesema bajeti ya TARURA imeongezeka kutoka shilingi bilioni 272.5 kwa mwaka wa fedha 2020/2021 hadi kufikia Shilingi bilioni 802.29 kwa mwaka wa fedha 2021/2022 sawa na ongezeko la asilimia 194.4, hadi kufikia tarehe 31 Desemba,2022 fedha kiasi cha shilingi bilioni 327.761 sawa na asilimia 41 zimepokelewa kwa ajili ya TARURA. 

Amesema pamoja na ongezeko hilo bado TARURA inahitaji kuongezewa fedha zaidi ili kukidhi mahitaji ya mtandao wa barabara wenye jumla ya Kilomita 144,429.77 kutoka mtandao wa awali uliokuwa na kilomita 108,946.18
Share To:

Post A Comment: