Na Denis Chambi, Tanga. 

Umoja wa wanawake Tanzania wa chama cha mapinduzi 'CCM' Taifa kimempongeza rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maamuzi aliyoyafanya ya kundoa zuio na kuruhusu mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa hapa nchini jambo ambalo linaonyesha kuendelea kukua kwa Demoktasia. 

Pongezi hizo zimetolewa na mwenyekiti wa UWT Taifa Merry Chatanda mkoani Tanga ikiwa ni siku moja tu mara baada ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassani kuondoa vikwazo vilivyokuwepo vikizuia vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara hapa nchini, kukwamua mchakato wa kuapatikana kwa katiba mpya pamoja na kufanyika marekebisho ya sheria mbalimbali katika sera ya uchaguzi.

 "UWT Taifa inampongeza sana Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kufanya maamuzi yaliyotokana na mkutano wa pamoja uliofanyika baina ya Rais na viongozi a vyama vya siasa kwa kufanya maamuzi yaliyoleta furaha isiyokuwa na kifani kwa wananchi wa Tanzania na wapenda amani dunia kote kwa kutoa majawabu ya vikwazo vya demokrasia yetu sisi kama UWT tumekoshwa sana na hatua ya kihistoria kuondoa zuio la mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa , kukwamu mchakato kwa kupata katiba mpya na kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali ili kutanua wigo wa demokrasi hapa nchini maamuzi haya yameleta faraja kwa vyama vya siasa hapa nchini" alisema Chatanda.

 "Hakika kwa maamuzi aliyoyafanya Rais kupitia mchakato wa maridhiano kwa kuundwa kikosi kazi na pia mazungumzo kati ya vyama vya CCM na CHADEMA yameleta matumaini mapya katika kujenga demokrasia ya kuaminiana ambayo ni chachu ya kujenga taifa lenye umoja amani na utuluivu" aliongeza. 

Aidha Chatanda amevitaka vyama vya siasa vyote hapa nchini kutumia vyema mikutano ya hadhara kwa wananchi kwajili ya kuifanya mikutano yenye tija kwa jamii na maslahi mapana ya Taifa na kuachana na kashfa na kejeri ambazo hazina tija kwa maendeleo ya Tanzania. 


"Umoja wa wanawake Tanzania unaungana na wito wa Mheshimiwa Rais kwa wana siasa kutumia mikutanio ya hadhara vizuri kwa kufanya mikutano na siasa za kistaarabu zenye kujenga na kuacha matusi na kashfa rais wetu ni kiongozi msikivu na mpenda haki na ndio maana maamuzi aliyoyatoa ni mwelekeio mpuya katika kuihami demokrasia yetu " alisema mwenyekiti huyo. 

Pamoja na hayo Chatanda amewataka viongozi wanawake wa siasa kuonyesha utu katika mikutano ya hadhara pamoja na kunadaa mikutano mingi itakayolenga kuangazia changamoto zinazowakumba wanawakwe hapa nchini na hatimaye kuweza kumkomboa katika nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii.

 "Umoja wa wanawake Tanzania 'UWT' inawasisitiza sana viongozi wanawake ndani ya vyama mbalimbali vya siasa kuandaa mikutano mingi ya hadhara ili kuweza kupokea changamoto mbalimbali zinazowakumba wanwake kwa kuwa wanawake wengi wa Tanzania wanakabiliwa na changamoto zinazofanana bila kujali itikadi zao na pia katika mikutano hiyo tupendekeze hatua mahususi za kuchukuliwa na serikali ili tuweze kumkomboa mwanamke kiuchumi , kijamii na kisiasa" alisema Chatanda. 

Mwenyekiti wa chama cha wananchi 'CUF' wilaya ya Tanga Khamis Mnyeto amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kufwatia hatua hiyo ambapo alisema ni jambo la mfano na kuigwa na amefungua milango kwa vyama pinzani ambayo iliyokuwa imefungwa kwa muda mrefu na kuthibitisha kuwa uwepo wao utachagia ukuwaji wa demokrasia na maendeloe endelevu ya Taifa zima. 


"Hili ni jambo jema kwa sababu ilikuwa tayari vyama vya siasa vimeshazimia lakini jambo hili nadhani amefahamu kuwa nyumba inayojengwa ni moja hivyo hakuna haja ya kuendelea kugombani fito kwahiyo akaamu kurudisha demokrasi kusema kweli kwa hili nimpongeze sana na ninaomba aupokee ukosoaji wetu na aufanyie kazi nina hakika ukosaji wetu utakuwa ni wakujkenga sio wa kubomoa bali ni kujenga vitu ambavyo ni stahiki ya watanzania" alisema Mnyeto . 

Aliewahi kuwa mbunge wa jimbo la Tanga mjini kwa tiketi ya chama cha Wananchi 'CUF' Mussa Mbaruku naye alipongeza hatua hiyo ambayo inaonyesha kuendelea kwa demokrasia hapa nchini huku akiwataka viongozi wa vyama vya siasa vyote hapa nchini kutanguliza maslahi mapana ya Taifa huku wakishauri mambio ambayo yatazidi kuchochea maendeleo. 

"Nimpongeze kwa fikra na busara sana kwa Rais kwa sababu hili ni jamblo la kisheria lakini tutambue kwamba Tanzania sio kisiwa na wakati wote huko tulikotoka kulikuwa kumwezuiwa mikutano na maandamano na hii ilitufanya wanasiasa tukawa waoga lakini naamini kwa kuruhusiwa mikutano nawakumbusha wenzangu kuwa Tanzania kwanza na vyama vyetu baadaye kuwa fursa hii iliyotolewa tuitumie vizuri kwa kutumia busara na hekima" alisema Mbaruku. 

Mwenyekiti wa chama cha wananchi 'CUF' wilaya ya Tanga Khamis Mnyeko.
Aliewahi kuwa mbunge wa jimbo la Tanga mjini kwa tiketi ya chama cha Wananchi 'CUF' Mussa Mbaruku.

Share To:

Post A Comment: