Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM taifa Fadhili Maganya amesema kuwa safari za nje ya nchi za  Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu zinamaslahi makubwa na nchi kwani zinafungua njia katika utekelezaji ya miradi mbalimbali yaaendeleo.

Maganya aliyasema hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari mkoa wa Arusha wa kutoa tamko la umoja huu kwa Rais ambapo alisema kuwa anapokwenda nje ya nchi harudi bure kuna fedha nchi inapata ikiwemo ile ya UVIKO-19 ambayo imepelekea kutuliza kelele za madarasa kwa wanafunzi wanaojiunga na kidato cha kwanza.

“Tumpe sapoti, tumuache asafari anatufungulia njia “mwenda bure sio sawa na mkaa bure huwenda akaokota”,“mguu mtembezi usiporudi na umande unarudi na mwiba”kwahiyo safari za mama nje ya nchi zinamaslahi kwa nchi yetu, tunapata mikopo kwaajili ya maendeleo hakuna mradi uliosimama wala hakuna mtoto ambaye hatoenda shule kwasababu ya ufinyu wa madarasa,” Alisema Maganya.

Alifafanua kuwa miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa nchini kuna ambayo inatelelezwa kwa kodi za watanzania lakini pia ipo inayotekelezwa kwa mikopo ambayo nchi inapata kutoka nje kwa juhudi za Mh Rais anaposafiri kwenda huko.
Aidha kuhusiana na mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa alitoa wito kwa vyama vya siasa kutumia mikutano hiyo kujenga nchi lakini pia watanzania kumtia moyo na kuunga mkono kwa uamuzi huo kwani umoja na mshikamano ndio msingi wa maendeleo katika nchi.

“Umoja wa wazazi unaviomba vyama vya siasa kuzingatia sheria na kanuni na miongozo mbalimbali katika utekelezaji wa shughuli za siasa hapa nchini na kwa pamoja tuumunge mkono Rais kwa kuendeleza siasa za maridhiano kwa maslahi mapana na mustakabali wa nchi yetu,” Alisema Maganya.

Sambamba na hayo jumuiya hiyo imempongeza na kumuunga mkono Rais kwa kuonyesha uongozi madhubuti na imara ambao unaendelea kufanya nchi kuwa na amani na utulivu ambayo ni kuanzisha siasa za maridhiano, mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa, kuanza kukwamua mchakato wa katiba pamoja na kuendelea kuangalia sheria mbalimbali kwaajili ya kuziboresha.
Share To:

Post A Comment: