MKUU wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akizungumza kwenye kikao cha pamoja na Viongozi wa Vyama vya Siasa Mkoa wa Dodoma wakati wakijadili utekelezaji wa agizo  lililotolewa hivi karibbu  na Rais Samia kuruhusu vyama vya Siasa nchini kufanya Mikutano ya hadhara.

 

Sehemu ya Wakuu wa Wilaya ya Dodoma pamoja na Viongozi wa Usalama wakimsikiliza Mkuu  wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule (hayupo pichani) kwenye kikao cha pamoja na Viongozi wa Vyama vya Siasa Mkoa wa Dodoma wakati wakijadili utekelezaji wa agizo  lililotolewa hivi karibbu  na Rais Samia kuruhusu vyama vya Siasa nchini kufanya Mikutano ya hadhara.

KAMANDA  wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Martin Otieno,akijibu hoja mbalimbali zilizotolewa na Viongozi wa Vyama vya Siasa Mkoa wa Dodoma wakati wa  kikao cha pamoja na Viongozi wa Vyama vya Siasa Mkoa wa Dodoma kujadili  utekelezaji wa agizo  lililotolewa hivi karibbu  na Rais Samia kuruhusu vyama vya Siasa nchini kufanya Mikutano ya hadhara.

KATIBU  wa Chama cha Wananchi (CUF), Yusuf Nassoro,akichangia hoja wakati wa kikao cha pamoja na Viongozi wa Vyama vya Siasa Mkoa wa Dodoma chenye lengo la kujadili  utekelezaji wa agizo lililotolewa hivi karibbu  na Rais Samia la  kuruhusu vyama vya Siasa nchini kufanya Mikutano ya hadhara.

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dodoma (CHADEMA), Mathias Nyakapala,akichangia hoja wakati wa kikao cha pamoja na Viongozi wa Vyama vya Siasa Mkoa wa Dodoma chenye lengo la kujadili  utekelezaji wa agizo lililotolewa hivi karibbu  na Rais Samia la  kuruhusu vyama vya Siasa nchini kufanya Mikutano ya hadhara.

Mwenyeikiti wa Chama cha Demokrasia Makini mkoa wa Dodoma, Baraka Machumua ,akichangia hoja wakati wa kikao cha pamoja na Viongozi wa Vyama vya Siasa Mkoa wa Dodoma chenye lengo la kujadili  utekelezaji wa agizo lililotolewa hivi karibbu  na Rais Samia la  kuruhusu vyama vya Siasa nchini kufanya Mikutano ya hadhara.

KATIBU wa Chama cha TLP Mkoa wa Dodoma Bi.Damaly Richard,akichangia hoja wakati wa kikao cha pamoja na Viongozi wa Vyama vya Siasa Mkoa wa Dodoma chenye lengo la kujadili  utekelezaji wa agizo lililotolewa hivi karibbu  na Rais Samia la  kuruhusu vyama vya Siasa nchini kufanya Mikutano ya hadhara.

Mwenyeiki wa NCCR-Mageuzi, Meshack Masinga,akichangia hoja wakati wa kikao cha pamoja na Viongozi wa Vyama vya Siasa Mkoa wa Dodoma chenye lengo la kujadili  utekelezaji wa agizo lililotolewa hivi karibbu  na Rais Samia la  kuruhusu vyama vya Siasa nchini kufanya Mikutano ya hadhara.

Mjumbe wa NEC  Mkoa wa Dodoma kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM),Donard Mejeti ,akichangia hoja wakati wa kikao cha pamoja na Viongozi wa Vyama vya Siasa Mkoa wa Dodoma chenye lengo la kujadili  utekelezaji wa agizo lililotolewa hivi karibbu  na Rais Samia la  kuruhusu vyama vya Siasa nchini kufanya Mikutano ya hadhara.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Vyama vya Siasa Mkoa wa Dodoma mara baada ya kumalizika kwa kikao cha pamoja cha kujadili utekelezaji wa agizo lililotolewa hivi karibbu  na Rais Samia la kuruhusu vyama vya Siasa nchini kufanya Mikutano ya hadhara.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akiwa katika picha ya pamoja na Wakuu wa Wilaya Mkoa wa Dodoma wakati wa kikao cha pamoja na  Viongozi wa Vyama vya Siasa Mkoa wa Dodoma.

MKUU wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akiwa katika picha ya pamoja na Menejimenti ya Mkoa wa Dodoma mara baada ya kumalizika kwa  kikao cha pamoja na  Viongozi wa Vyama vya Siasa Mkoa wa Dodoma.


VIONGOZI wa Vyama vya Siasa 14 vya Mkoa wa Dodoma wamepongeza hatua ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu vyama kufanya Mikutano ya hadhara huku wakiahidi kufanya siasa za kistaarabu katika kulitumikia Taifa.

Viongozi wa vyama vya siasa mkoa wa Dodoma walibainisha hayo jleo Januari 5,2023 jijini Dodoma wakati wa Kikao  cha pamoja na Mkuu wa mkoa wa Dodoma , Rosemary Senyamule,wakati wakijadili utekelezaji wa agizo hilo lililotolewa hivi karibuni na Rais Samia.

Akichangia Mwenyeiki wa NCCR-Mageuzi, Meshack Masinga pamoja na kumshukuru Rais amesema kuwa NCCR-Mageuzi itaunga mkono uongozi wa Serikali iliyopo madarakani.

Amesema kuwa vyama pinzani ni kioo cha chama kilichopo madarakani kutokana na kukosoa pale kinapokosea kwa maslahi mapana ya taifa.

“Sisi ni wapinzani siyo maadui wa nchi tunaomba tupewe uwanja sawa wa kisiasa kwakuwa CCM, haijapangiwa kutawala nchi hii maisha kuna nchi wapinzani wameingia madarakani baada ya miaka 200 hivyo hata sisi ipo siku tutaingia na nyie CCM mtakuwa chama pinzani”amesema

Hata hivyo amefafanua kuwa  NCCR Mageuzi haitakuwa tayari kumfumbia macho mtu yeyote ambaye atavunja sheria ya vyama vya siasa nchini.

Kwa upande wake  Mjumbe wa NEC  Mkoa wa Dodoma kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM),Donard Mejeti ,ameahidi kufanya siasa za kistaarabu na kuvisihi vyama vingine kukosoa na kutoa maoni kwa luhha za kistaarabu.

“Kama milivyosema nyinyi kweli ni kioo chetu sisi tunajisifia tuu lakini nyinyi ndiyo mnaweza kutukosoa hivyo nawahakikishieni kuwa CCM mkoa wa Dodoma, tutafanya siasa za kistarabu”amesema

Naye Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dodoma (CHADEMA), Mathias Nyakapala,amemshukuru Rais Samia kuruhusu mikutano ambayo  ni msingi wa amani hasa wakati wa chaguzi na kusisitiza haja ya kupata Katibu Mpya, kuwa na Tume huru ya uchaguzi na kuzifanyia marekebisho sheria kandamizi za uchaguzi.

Mwenyeikiti wa Chama cha Demokrasia Makini mkoa wa Dodoma, Baraka Machumua amepongeza hatua ya Rais Samia kuruhusu mikutano ya hadhara na kusisitiza kuwa bila kuwapo mikutano hiyo ni ngumu kwa vyaka kuzalisha wanachama.

Naye Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma, Martin Otieno, amesema kuwa jeshi hilo halitakuwa kikwazo kwa chama chochote bali litatoa ushirikiano kwa kila chama bila kujali ukubwa wake.

“Tutatoa ushirikiano,vibali na ulinzi kwa chama chochote ambacho kitahitaji kufanya mkutano wake wa hadhara, kinachotakiwa ni kufuata na kuzingatia sheria za nchi”almesema

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule,amewaagiza viongozi wote ambao wapo chini yake kuhakikisha wanazingatia na kuyatekeleza maelekezo yote yaliyotolewa na Rais Samia.

”Nawaelekeza watendaji wa mkoa wangu kuhakikisha wanatekeleza maelekezo yote ya Rais Samia kwa kutoa ushirikiano kwa vyama vyote vilivyopo katika Mkoa huu hivyo nawaomba Viongozi wa vyama kwenda kuwaeleza wananchi wa Dodoma maendeleo yaliyipo katika Mkoa wao”amesema

Share To:

Post A Comment: